Mfanyabiashara wa Ufuta mjini Dodoma akipima magunia ya zao hilo kama alivyokutwa katika eneo la Communication Centre. Wafanyabiashara hao wanailalamikia Manispaa ya Dodoma kwa usumbufu wanaowapa wa kuzuia magari kushusha nafaka aina yeyote kiasi cha wao sasa kufanya shughuli hiyo kwa kujiiba na pindi wanapo kamatwa wamekuwa wakitakiwa kulipa faini ya hata shilingi laki tano kwa gari. Wanadai hali hiyo ina zaidi ya Mwezi mmoja sasa lakini pia wanashangaa wenzao waliopo eneo la Majengo kuruhusiwa kushusha nafaka na kuuza.
Sehemu ya marobota ya Ufuta yaliyopo katika eneo hilo lakini wanadai upakuaji wake hufanyika kwa kujificha.
Kuli akipakua robota la Ufuta kutoka katika gari.
0 comments:
Post a Comment