Miss Africa Crown Scandinavia 2010, Michelle Jeng amewasili nchini leo akitokea nchini Sweden anakoishi.
Michelle ambaye ni Mtanzania alitwaa taji hilo mwaka jana katika shibndano lililofanyika nchini Sweden na kushirikisha warembo 53 kutoka nchi za Kiafrika na wanaoishi nchi za Scandinavia.
Akiwa Nchini Mrembo huyo atafanya shughuli mbalimbali za kijamii ikiwa ni pamoja na kuwatembelea wenyeulemavu, waathirika wa mabomu Gongo la Mboto na kutembelea vituo vya watoto yatima mjini Dodoma pamoja na kutambulishwa Bungeni mjini Dodoma.
Miss Africa Crown Scandinavia, Michelle Jeng akiwasili nje ya uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam jana na kulakiwa na mamia ya wakazi wa Dar es Salaam.
Michelle akivaa taji lake alilovikwa katika mashindano hayo baada ya kutoka nje ya uwanja.
Miss Michelle akivishwa vazi la asili na Mwanaharakati wa Elimu nchini, Nderakindo Kessy baada ya kuwasili nchini.
Miss Michelle akipokea zawadi ya ua kutoka kwa mmoja wa watoto waliompokea. Katikati ni baba mlezi wa Michelle ambaye pia ni Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi Taifa, Joseph Mbatia.
Pia alipokea Bendera ndogo ya mezani ya Tanzania kutoka kwa watoto hao.
Ofisa Habari Kutoka Idara ya Habari Maelezo akimwongoza kushuhudia ngoma ya utamaduni wa Mtanzania iliyoandaliwa kwaajili yake.
Hapa wachezaji wa ngoma wa kikundi cha Ayatoru kutoka kule Mburahati Mianzini wakimzunguka kwa furaha wakicheza.
Vijana hawa nao wa Ayatoru nao waliona watoe pongezi zao na kumkaribisha mgeni.
Miss Michelle akipunga mkono kusalimia watu mbalimbali waliofika kumpokea.
Michelle (kushoto) akisikiliza risala iliyoandaliwa na Andrew James Mbatia na iliyosomwa kwake na Mwanaharakati Nderakindo Kessy uwanjani hapo.
Mrembo huyu pia nae alipata fursa ya kuzungumza na waandishi wa habari waliofika katika mapokezi hayo.
Wanahabari wakimfanyia mahojiano Mrembo huyo. Pia Juni 16, 2011 majira ya saa nne asubuhi katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo Dar es Salaam Michelle atazungumza na Wanahabari juu ya alichokifanya Nchini Kenya na Uganda.
0 comments:
Post a Comment