Nafasi Ya Matangazo

June 08, 2011

LEO ni leo mjini Dodoma pale Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo Pichani atakapowasili Bungeni majira ya jioni kusoma Bajeti ya Serikali katika kipindi cha 2011/2012.

Bajeti hiyo inasubiriwa kwa hamu kubwa na umma wa watanzania, huku matarajio ya kila mwananchi yakiwa ni bajeti ya kupunguza makali ya maisha, vyakula, mafuta na matumizi mengine yanatarajiwa kushuka na pia kutangazwa kwa nyongeza ya miashara licha ya kuwa Wafanyabiashara nao wanasubiri hioyo nyongeza wapandishe bei ya vitu.

Je serikali itaweka kipaumbele katika sekta ipi, na bajeti ya 2010/2011 ilifanikiwa kiasi gani kutekelezwa na watendaji wa sertikali?. Matumizi yasiyo yalazima bado yatakuwepo?.

Msikose kuungana na Blogu hii hapo baade nitawaopasha mengi na kuwapa picha za tukio hilo mjini Dodoma.
Posted by MROKI On Wednesday, June 08, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo