Kaimu Meneja masoko wa Zantel Brian Karokola (kushoto) akizungumza na wakati wa uzinduzi wa promosheni mpya ya ZARI SMS ambayo wateja wa Zantel watajishindia TSH milioni 1 kila siku, muda wa maongezi, simu aina ya Blackberry na laptop. Kulia nia Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano Zantel William Mpinga.
Dar es Salaam, Mei 12, 2011: Baada ya Hamisi Ma SMS kugawa mamilioni ya shilingi kampuni ya simu za mikononi ya Zantel kwa mara nyingine tena leo imezinduwa promoshen mpya kubwa inayojulikana kama ZARI SMS. Promoshen ya ZARI SMS itatoa jumla ya zawadi zenye thamani ya Tsh 160 milioni zitatolewa
kwenye droo za kila siku, kila wiki na kila mwezi. Promoshen ya ZARI SMS itafanyika kwa muda wa siku 84 na wateja zaidi ya 4,000 watajishindia Zawadi tofauti katika promoshenhii.
Kaimu Mkurugenzi wa Masoko wa Zantel Brian Karokola akizungumza na waandishi wa habari leo alisema nia ya kuanzisha promosheni hii ni kuwashukuru wateja wao wa Zantel na kuwapa fursa kujishindia Zawadi tofauti. “Promosheni ya ZARI tunaamini itabadili maisha ya wateja wetu kwa njia moja au nyingine kupitia awadi tulizowaandalia kama pesa taslim,simu aina ya Blackberry na laptop ambazo tayari zimeunganishwa na intaneti kwa mwaka mzima.”
Kushiriki kwenye promosheni ya ZARI SMS mteja wa Zantel anatuma SMS yenye neno ZARI kwenda 15587 na utapata nafasi ya kujishindia Tsh milioni 1 kila siku kwa mshindi mmoja kupitia droo, Tsh milioni 2 kila wiki kwa mshindi mmoja aliyetuma SMS nyingi zaidi na Tsh millioni 10 kwa washindi 10 mwisho wa
promoshen.
Vile vile mteja wa Zantel kupitia promosheni ya ZARI SMS anaweza kupata zawadi za papo hapo kama vile muda wa maongezi wa Tsh 5000 kwa watu 50 kila siku, simu aina ya Blackberry 1 kila baada ya siku moja na Blackberry 3 zitatolewa mwisho wa promoshen na Laptop 1 iliyoonganishwa na huduma ya internet kwa mwaka mzima kila wiki.
Kwa maelezo zaidi:
sharoncosta@zantel.co.tz 0776 491307




0 comments:
Post a Comment