Wanachma wa CCM na Wananchi wakazi wa jijini Dar es Salaam, wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa marehemu Athuman Hassan Mwinyimvua, aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, aliyefariki dunia leo, Mwinyimvua amezikwa leo Mei 20, kwenye Makaburi ya Karume Mwembechai. Maziko hayo pia yalihudhuriwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal.
Waumini wa Dini ya kiislamu wakibeba jeneza lenye mwili wa marehemu, Athuman Hassan Mwinyimvua, baada swala ya mwisho iliyofanyika katika Msikiti wa Mwembechai Dar es Salaam leo Mei 20, Mwinyimvua alifariki dunia leo na kuzikwa katika makaburi ya Karume Mwembechai Dar es Salaam.
Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka mchanga kwenye kaburi la aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Athumani Hassan Mwinyimvua, aliyefariki dunia leo na kuzikwa leo Mei 20 kwenye Makaburi ya Karume Mwembechai.
0 comments:
Post a Comment