Bi Harusi Mtarajiwa Asha Ramadhani Ng'humbi (kushoto) akiwa na Msimamizi wake Bi. Maria Kaluse wakati wa tafrija yake ya kumpongeza na kumtakia baraka baada ya kuiambia familia yake kuwa amepata mchumba na anataraji kufunga ndoa yao Takatifu Mei 28, 2011 jijini Dar es Salaam. Tafrija hii ilifanyika katika Ukumbi wa Makuti-JWTZ Msasani Beach Club, usiku wa Mei 20,2011.
Bi Harusi Mtarajiwa Asha akiwa katika picha ya pamoja na Mumewe Mtarajiwa Bwana George Bonzo wakati wa tafrija hiyo.
Asha akipeleka keki kwa wazazi ikiwa ni shukrani yake kwao kwa malezi.
Christina Manongi "Sinta" ambae ni dada wa Asha akisaidia kupeleka keki iliyokatwa kwaajili ya waalikwa wote ukumbini.
Asha akigonganisha glasi za wine na mpambe wake Maria.
Baba wa Asha, Mzee Ramadhani Ng'humbi akisema neno kwa wageni waalikwa katika tafrija ya binti yake. Kushoto ni Mkewe Mheshimiwa DC Bukombe, Hawa Ng'humbi.
MKUU wa Wilaya ya Bukombe mkoani Shinyanga, Hawa Ng'umbi ambae ni mama mzazi wa Asha, akisema machache kwa Binti yake.
Baadhi ya wageni waalikwa katika tafrija hiyo wakifuatilia matukio.
Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Kinondoni, Emmanuel Makene Tamila nae alikuwepo katika tafrija hiyo, kushoto ni Mkurugenzi wa MD Digital Company, Debora Fute.
Mhadhiri wa Chuo Cha Mipango Dodoma, Shauri Timoth Kaluse ambae ni kaka wa Asha akicheza nae mziki ukumbini.
Ulikuwa ni muda muafaka wa msosi hivyo George alikuwa karibu na mamaa.
Wageni wakipata chakula maalum kilichoandaliwa kwaajili ya kumpongeza Asha.
Victoria Kaluse (kulia) akiwa na Wifi yake Gudila Tarimo nao wakipata vitu roho inapenda.
Kaka Sixtus Mapunda nae aliwakilisha, hapa akiteta jambo na Mheshimiwa Hawa na Mumewe Mzee Ng'umbi.
Wageni waalikwa walimpongeza Mheshimiwa Hawa Ng'umbi kwa malezi na kuozesha binti yake.
0 comments:
Post a Comment