Yaamemfika mauti,
Mtabiri madhubuti,
Imekatika sauti,
Yahaya bin Huseni.
Alisifika maskani,
Nanchi za majirani,
Atakumbukwa nchini,
Limetutoka jabali.
Sifaze kwa Maulana,
Huenda zisimpe lana,
Amjalie Karima,
Mahali panapo faa.
Sijui yake majini,
Atakaerithi nani,
Yasije enda mtaani,
Kwaheri Yahaya Nenda.
Hi leo alifajiri,
Mwanae ameshakiri,
Bin Yahaya Kasafiri,
Buriani Shehe wetu.
Alitabiri vitu vingi,
Mtwara hadi Usangi,
Na hakubagua rangi,
We tangulia Yahaya.
Machozi yananitoka,
Shukrani ulotukuka,
Jalalu usotuchoka,
Mlaze pema Yahaya.
(C)Mroki Mroki "Father Kidevu"
Mtabiri Maarufu Afrika Mashariki na Kati, Sheikh Yahya Husein amefariki jijini Dar es Salaam leo.
0 comments:
Post a Comment