Baadhi ya washiriki wa shindano la Vodacom Miss Tabzata 2011.
Na Mwandishi Wetu
Kinyang’ajiro cha kumsaka Miss Tabata 2011 kinatarajia kufanyika Juni 10 katika ukumbi wa Da’ West Park.
Mratibu wa shindano hilo Joseph Kapinga amesema jana kuwa warembo 25 wanajianda kushindania taji hilo.
“Mpaka sasa tumebaki na warembo 25 bomba baada ya kuwachuja 17,” Kapinga alisema.
Kapinga alisema warembo hao wanaoendelea na mazoezi katika ukumbi Da’ West Park, Tabata chini ya mkufunzi Joyce Joseph Kaniki.
Warembo wanaoendele na mazoezi ni Marion Augustino (19), Lucy Mboya (21), Neema Marwa (18), Catherine Julius (20), Hawa Rajabu (19), Lilian William (20), Godliver Mashamba (22) na Dorice Mutabingwa (21).
Wengine ni Sweetlily Suleiman (21), Maria John (21), Happyness Emmanuel (18), Cresensia Haule (20), Mariam Manyanya (21), Angela Benard (18), Agustina Mshanga (20), Nasra Salim (21), Faiza Ally (19), Mgayo Haruna (21) na Edina Mnada (21).
Pia wamo Angela Fortunatus (21), Lucia Joseph (20), Neema Mwakibinga (21), Lilian Brayson (22), Rita Mvungi (21) na Willieth Wilson (22).
Miss Tabata 2011 inadhaminiwa na Dodoma Wine, Vodacom, Redds Original, Integrated Communications, Paris Pub, Fabak Fashion, Freditto Entertainment, Chicken Hut, Travel Partners, Ben Expedition, Screen Masters, Sean Entertainment, Screen Masters na Michuzi blogspot.
Consolata Lukosi ndiye mrembo anayeshikilia taji la Miss Tabata. Consolata alikuwa nambari tatu mwaka jana kwenye shindano la taifa (Vodacom Miss Tanzania) kabla ya kushinda taji la Redds Ambassador.
Miss Tabata inaandaliwa na Bob Entertainment na Keen Arts.
0 comments:
Post a Comment