Nafasi Ya Matangazo

May 29, 2011


Mmoja wa waendeshaji wa shindano la Serengeti dansi la fiesta 2011,Babuu wa kitaa ambaye pia ni mtangazaji wa Clouds TV,akisoma makundi yatakayochuana leo jioni,katika suala zima la kumsaka mkali wa msimu wa dhahabu unaoendelea na Serengeti dansi la fiesta 2011,ndani ya mji wa Morogoro.
 Kikundi cha Cabo Red kikionesha umahiri wake wa kuyarudi mangoma jioni ya leo wakati wa shindano la kumsaka kinara wa msimu wa dhahabu unaoendelea na Serengeti dansi la Fiesta ndani ya mkoa wa Morogoro,ama kwa hakika ushindani na ubunifu ulikuwa mkubwa kwa makundi yote yaliyoshiriki.
 Kikundi cha Moro Skwadi kikionyesha manjonjo yake ya kusakata dansi mbele ya mashabiki (hawapo pichani),jioni ya leo kwenye ukumbi wa maraha wa For Star,wakati wa kumsaka kinara wa msimu wa dhahabu unaoendelea na Serengeti dansi la fiesta 2011.
 Kundi la Gentlemen likiwa stejini likirusha karata yake jioni ya leo katika ukumbi wa For Star,katika lile shindano la kumsaka mkali wa msimu wa Dhahabu unaoendelea na Serengeti dansi la Fiesta ndani ya mkoa wa Morogoro.
 Kundi pekee ambalo pia liliwashirikisaha akina dada wawili,liitwalo  Morogoro Youth Universe of  Talents, (MYUT) likiwajibika vilivyo stejini kwa namna ya kipekee kabisa,hali iliyopelekea ukumbi ulipukwe na mayowe na miluzi kila wakati,kutokana kundi hilo kuonesha umahiri mkubwa wa kucheza,kwenye shindano la kumsaka kinara wa msimu wa dhahabu unaoendelea na Serengeti dansi la fiesta 2011 ndani ya Mji kasoro bahari a.k.a Morogoro.
 Kikundi cha Cabo Red kikionesha umahiri wake wa kucheza staili ya Michael Jakson kupitia wimbo wake wa Thriller jioni ya leo.
 Kundi la Morogoro Youth Universe of  Talents, (MYUT),likishangilia kwa kishindo huku kila mmoja akimbeba mwenzake kwa furaha kubwa,mara baada ya kuibuka washindi wa shindano la kumsaka mkali wa msimu wa dhahabu unaoendelea na Serengeti dansi la fiesta 2011.
 Meneja matukio wa kanda ya Kusini wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL),Bwa.Albert Nsanzugwanko akilikabidhi kundi liitwalo  Gentlemen fulana za Serengti kwa kila mmoja,ambalo lilifanikiwa kufanya vyema na kushika nafasi ya pili.
Kundi la Morogoro Youth Universe of  Talents, (MYUT) likiwa limekabidhiwa kreti ya bia ya Serengeti ikiwa ni sehemu ya zawadi yao kwa kufanya vyema katika shindano la kulisaka kundi kinara la msimu wa dhahabu unaoendelea na Serengeti dansi la fiesta 2011,ambalo limefanyika jioni ya leo kwenye ukumbi wa Four Stars,Morogoro.
Posted by MROKI On Sunday, May 29, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo