Nafasi Ya Matangazo

May 26, 2011

Habari za hivi punde kutoka Gongo la Mboto zinasema Kikosi cha JWTZ 511KJ-Gongolamboto kinapita mtaani kikitoa taarifa ya kuwapo kwa milipuko mipya leo hii ikiwa ni zoezi la kuteketeza baadhi ya mabomu yaliyosalia baada ya kulipuka kwa maghala kadhaa ya mabomu katika kambi hiyo.

Wakipita na vipaza sauiti katika gari na kuwaomba wananchi kuwa watulivu katika muda huo ambao mabomu yatakuwa yakilipuka ambapo ni wakati wowote kuanzia mchana huu.

Februari 17, 2011 majira ya saa mbili usiku palitokea milipuko ya mabomu kwenye ghala la kuhifadhia silaha huko Gongolamboto, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Posted by MROKI On Thursday, May 26, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo