Nafasi Ya Matangazo

July 09, 2010

Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Tanzania Ephraim Mafuru akifafanua jambo wakati akiitambulisha huduma mpya ya ‘NIPIGE TAFU’ itayomuwezesha mteja wa kampuni hiyo kuomba salio la shilingi 500/- kutoka Vodacom kwa kupiga namba *150*05# kwenye semina iliyoandaliwa kwa wahariri wa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam Julai 8 2010.

Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania imezindua huduma mpya ya “NIPIGE TAFU” huduma inayomwezesha mteja wa Vodacom wa malipo ya kabla na Vodajaza kuomba muda wa maongezi akiwa ameishiwa na salio na anahitaji kupiga simu ya dharura.

Huduma hii ya kipekee sit u inaweka Vodacom kama kinara wa Mawasiliano Tanzania bali inaonyesha ni jinsi gani kampuni hii inajali wateja wake kwa hali na mali haswa pale wanapokuwa wamekwama.

Kuomba muda wa maongezi,mteja anapaswa kupiga namba *150*05# na Vodacom itamtumia muda wa maongezi kwa kiasi cha shilingi 500,na itakuja kumkata mteja shilingi 550 mara baada ya kuongeza salio lake,Shilingi 50 ni gharama ya huduma kutoka kwa mteja aliyeoomba msaada huo.

Mkurugenzi wa masoko wa Vodacom Tanzania Ephraim Mafuru alisema kuwa”huduma hii itasaidia sana wananchi na wateja waliojisajili kwani ni mara nyingi sana watu huwa wanakwama kwa namna moja au nyingine na wanahitaji msaada wa haraka”Mafuru aliendelea kusema kuwa tunafuraha sana kuweza kutoa huduma hii muhimu itakayowasaidia wateja wetu pindi wakiwa kwenye matatizo.Hii inaonyesha ni jinsi gani Vodacom inajali na kuthamini wateja wake”.

Huduma hii ikijumwishwa na huduma nyingine za Vodacom ka Habari Ndiyo Hii,Cheka time,Vodajamaa na M pesa na nyinginezo nyingi ndizo zinazofanya Vodacom Tanzania kuwa mtandao wenye gharama nafuu na huduma zilizo bora hapa nchini.

Posted by MROKI On Friday, July 09, 2010 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo