Nafasi Ya Matangazo

June 30, 2010

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizindua rasmi awamu ya kwanza ya ukarabati na upanuzi (Rehabilitation and extension) wa shule ya sekondari ya wasichana ya Tabora unaofanywa kwa hisani ya Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) uliogharimu zaidi ya shilingi bilioni 1.7. Kulia kwa Mama Salma ni Mkuu wa Shule hiyo Ms Agness Mlelwa na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ndugu Abeid Mwinyimsa. Uzinduzi huo ulifanyika tarehe 28.6.2010.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwapungia wanafunzi wa shule za sekondari za Tabora (wavulana na wasichana) na Milambo walihudhuria sherehe za upanuzi na ukarabati wa shule ya sekondari ya wasichana Tabora

Mama Salma Kikwete akitembelea moja ya bweni lililokarabatiwa katika shule ya wasichana ya Tabora mara tu baada ya kuzindua mradi wa ukarabati na upanuzi wa shule hiyo.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwahutubia mamia ya wanafunzi wa shule za sekondari za Tabora wavulana na wasichana na Mirambo wakati wa sherehe za uzinduzi wa upanuzi na ukarabati wa shule ya sekondari Tabora wasichana.
Posted by MROKI On Wednesday, June 30, 2010 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo