Nafasi Ya Matangazo

June 22, 2010



Soka la kila namna lilioneshwa katika Mashindano ya 32 ya UMISSETA yanayoendelea katika viwanja vya Shirika la Elimu Kibaha.
Mchuano hapa ulikuwa ni kati ya Kanda ya Kusini (nyeupe) na Kanda ya Magharibi. Wapo walio lamba vumbi na kubusu mpira bila kupenda, lakini ni sehemu ya kukuza vipaji maana vipo.
Unapo katwa mtama unaweza anguka vyovyote vile kama huyu aliyelambwa kimo cha mbuzi.
Magharibi (blue) walionesha kandanda safi sana lakini hawakuwa na bahati ya kumalizia vizuri kama Cameron. Nipatashika langoni mwa Kanda ya Magaribi lakini hapakuwa na goli kwa pande zote mbili hadi kipenga cha mwisho.
Mashabiki wa Kanda ya Magharibi wakishangilia timu yao ya mpira wa Mikono iliyokuwa ikiichakaza timu ya Kanda ya Nyanda za Juu. Hapakuwa na Mavuvuzela ni staili tu.
Huu ni mpira wa mikono Nyanda za Juu (nyeupe) akimenyana na Kanda ya Magharibi.
Mlinda mlango wa Kanda ya Nyanda za Juu akiokota moja ya mipira iliyotinga langoni kwake.
Mpira wa Kikapy ilikuwa ni patashika kati ya wasichana wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini na Kanda ya Kaskazini ambapo wadada wa Nyanda ya Juu Kusini walishinda kwa vikapu 31-25vya wapinzani wao. Furaha ya ushindi huja na staili za ushangiliaji.
Mchezo wa Volebal ilikuwa ni pata shika ya nguo kuchanika katia ya Kanda ya Ziwa na Kanda ya Ziwa Magharibi. Matokeo ni Kanda ya Ziwa walishinda kwa 25-17.
Maandalizi ya mashindano ya Riadha nayo yalikuwa yakifanyika kwa kuweka chokaa katika njia za kukimbilia.

Posted by MROKI On Tuesday, June 22, 2010 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo