Nafasi Ya Matangazo

June 22, 2010

Eneo la daraja la Kibamba nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam bado limekuwa ni eneo sugu la ajali za magari madogo na makubwa. Bado ipo katika akili za watu wengi hasa wakazi wa Kibamba na vitongongoji vyake pale watu kumi walipofariki katika ajali ya gari iliyolihusisha lori la mafuta na gari dogo la abiria. Leo majira ya saa 2 asubuhi lori hili pichani lilishindwa kupanda mlima na kurudi nyuma na derteva wake alifanikiwa kulikita katika mtaro kama linavyoonekana na kutoleta madhara kwa magari yaliyokuwa nyuma yake. Lori hili lilikuwa linaelekea maeneo ya Chalinze mkoani Pwani likitokea Jijini Dar es Salaam.
Posted by MROKI On Tuesday, June 22, 2010 1 comment

1 comment:

  1. AnonymousJune 23, 2010

    Ndugu mwana blogu hii kama unaweza kuwasiliana na watu wa TANROADS tafadhali wapelekee ujumbe huu. Eneo la Kibamba Darajani lina matatizo ya kiufundi katika ujenzi wake. Yale matuta mawili yaliyowekwa pande mbili za daraja ni mtihani mkubwa kwa malori ya mizigo, kwa kawa madereva wanalazimika kupunguza mwendo kabla ya kuvuka matuta hayo hali ambayo inasababisha kukosa nguvu ya kupanda mlima ulio mbele kwa kila upande. Ushauri wa bure: TANROADS ondoeni yale matuta zibakie rasta ambazo zinaztosha kabisa kuwakumbusha madereva kuwa mbele kuna daraja.

    ReplyDelete

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo