Askari wa zamani wa Kikosi cha KR 6, Captain David Nickol (katikati) akiwa na Mkewe kulia Aysha Nickol na Balozi wa Uingereza nchini Diane Corner alipo kwenda katika mnara wa Askari Posta Mpya Juni 16 2010 kuweka shada la maua kuwaenzi askari wenzake waliopigana vita kati ya mwaka 1939-1946. Mzee David akitoa heshima ya Kijeshi baada ya kuweka shada la maua.David Nikol akipiga picha na Balozi wa Uingereza Nchini Diane Corner. David akizungumza na waandishi baada ya zoezi hilo. Mzee huyu alizungumza kiswahili safi licha ya kuishi Uingereza tangu miaka hiyo ukoloni uondoke nchini.
Shada ambalo David Nikole ambaye anasema akiwa na kikosiu chake cha 6 KR alipigana katika nchi za Somalia, Uhabeshi, Madagaska na Barma aliliweka. Aidha shada hilo litawekwa pia katika Manara wa Mashujaa Mnazi Mmoja siku ya Mashujaa.
We Mroki we. Tafadhali waambie waliondoe hilo SHADA hapo haraka sana walipeleke Makumbusho ya Taifa, vinginevyo baada ya siku mbili tu hamtalikuta hapo. Vibaka wa Bongo wenyewe si mnawacheki?
We Mroki we. Tafadhali waambie waliondoe hilo SHADA hapo haraka sana walipeleke Makumbusho ya Taifa, vinginevyo baada ya siku mbili tu hamtalikuta hapo. Vibaka wa Bongo wenyewe si mnawacheki?
ReplyDeleteShauri zenu.
Mi ndo nshasema hivyo.