Hatimaye mrembo Neema Jamal,Aprili 30 alifanikiwa kulitwaa taji la Miss Chumbageni 2010 baada ya kuwabwaga warembo wengine 7 waliokuwa wakiwania taji hilo.
Mashindano hayo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa La Club Tanzanite Chuda Relini jijini Tanga na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watazamaji.
Mashindano hayo ambayo yalipambwa na burudani ya muziki kutoka bendi ya Bwagamoyo International inayoongozwa na Mwinjuma Muumini 'Kocha wa Dunia'.
Nafasi ya pili ilichukuliwa na Halima Salehe wakati nafasi ya tatu ilikamatwa na Chausiku Ibrahimu huku Taji la Kipaji likinyakuliwa na Agnes Mambo ambaye pia ni Mtangazaji wa Radio Mwambao Fm ya jijini Tanga.
Mashindano hayo yalikuwa ya ushindani mkubwa kutokana na warembo hao kuwa na vigezo vinavyokaribiana huku Agnes Mambo akiongoza kwa kushangiliwa na mashabiki waliohudhuria onesho hilo.
Kwa mujibu wa Mratibu wa Onesho hilo,Sussan Uhinga kutoka Kampuni ya Apple Partners mshindi wa kwanza alijinyakulia kitita cha shilingi 100,0000 huku mshindi wa pili na watu wakijinyakulia sh 50,000 huku washiriki wengine wakipata kifuta jasho cha sh.30,000 kila mmoja.
0 comments:
Post a Comment