Bondia wa timu ya AShanti ya Ilala. Matiku Magesa (kulia) akilusha ngumi kwa mpinzani wake, Hans John wa Klabu ya Sifa wakati wa mashindano ya kujipima nguvu kujiandaa na klabu bingwa yaliyofanyika Dar es salaam mwishoni mwa wiki, Hans alishinda kwa pointi 3.1.
Akizungumza Dar es salaam mwishoni mwa wiki wakati wa Mashindano ya kujipima uwezo yaliyoandaliwa na Klabu hiyo na kushirikisha klabu mbalimbali za wilaya hiyo, Katibu Mkuu wa BFT, Makore Mashaga alisema kutokana na nia nzuri inayooneshwa na klabu hiyo BFT itatoa ushirikiano ili kuendeleza mazuri hayo.
"Hii ni kazi nzuri, BFT tunafurahi kuona klabu kama Ashanti zinavyoonyesha uzalendo hili ni suala ambalo mimi naliunga mkono na panapowezekana tutatoa mchango wetu kwenu," alisema Makore.
Wakati huo huo Kocha wa Ashanti Rajabu Mhamila 'Super D' alisema mashindano hayo yataendelea kufanyika kila mwezi na kushirikisha klabu mbalimbali ili kuendeleza nia yao ya kukuza mchezo wa ngumi katika wilaya hiyo.
SHIRIKISHO la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT), limeipongeza klabu ya Ashanti kwa nia yake ya kuufufua mchezo wa ngumi katika Wilaya ya Ilala ambayo kwa muda mrefu ulionekana kupoteza mwelekeo wilayani humo.
Akizungumza Dar es salaam mwishoni mwa wiki wakati wa Mashindano ya kujipima uwezo yaliyoandaliwa na Klabu hiyo na kushirikisha klabu mbalimbali za wilaya hiyo, Katibu Mkuu wa BFT, Makore Mashaga alisema kutokana na nia nzuri inayooneshwa na klabu hiyo BFT itatoa ushirikiano ili kuendeleza mazuri hayo.
"Hii ni kazi nzuri, BFT tunafurahi kuona klabu kama Ashanti zinavyoonyesha uzalendo hili ni suala ambalo mimi naliunga mkono na panapowezekana tutatoa mchango wetu kwenu," alisema Makore.
Katibu huyo ambaye alikuwa mgeni mwalikwa katika mashindano hayo alizitaka klabu zingine za mchezo wa ngumi hapa nchini kuiga mfano wa klabu hiyo kwa kujiandalia michuano mbalimbali ambayo itawawezesha kujua viwango vya wachezaji wake mara kwa mara.
Wakati huo huo Kocha wa Ashanti Rajabu Mhamila 'Super D' alisema mashindano hayo yataendelea kufanyika kila mwezi na kushirikisha klabu mbalimbali ili kuendeleza nia yao ya kukuza mchezo wa ngumi katika wilaya hiyo.
Mashindano hayo yalishirikisha klabu za Sifa ya Manzese na Mtakuja ya Vingunguti ambapo mabondia Rajabu Hamisi wa Ahanti alimtwanga kwa point Joseph Meshack wa Sifa, Badru Hassan wa Ashanti alimdunda Salumu Iddi wa Mtakuja, Aseid Said wa Asanti alishindwa kutamba mbele ya Shabani Mafiga wa Sifa na Iddi Ramadhani wa Ashanti alimchakaza Kulwa Kiliani wa Mtakuja nae Iddi Pialali wa Sifa alimshinda kwa pointi Matiku Magesa wa Ashanti.
0 comments:
Post a Comment