Jamaa wanaolia na ujira wao akiwa mtaroni.Kaka, watu wengine hawana huruma wala utu.
Juzi nilipeleka gari yangu service katika gereji moja pale karibu na Mabibo Hostel, nikakuta shughuli ya uchimbaji wa mtaro ikiendelea, jamaa wametoka mijasho chepe. Ungedhani wana furaha kumbe huzuni tele moyoni.
T-Shirt yangu ya kazi mjomba ikanichongea.
Waliponiona tu wakanidaka. "Njoo kaka utusikilize huenda ukatufikishia kilio chetu". Nikawasogelea. Basi wakaanza."Kaka sisi hapa usituone hivi tunapigika na hizi kazi ngumu lakini ujira wetu wala hatuupati kama inavyopaswa.
Makubaliano yetu ni kulipwa kila tukimaliza ngwe tuliyopimiwa ambayo mara nyingi huwa ni urefu mita 10 x kina futi 5, sh. 2,000 kwa mita. Tumemaliza hizo ngwe nyingi tu lakini hadi sasa malipo yetu tunapigwa danadana tu".
Ndipo nikawapiga picha hizi, nikawaeleza kuhusu masuala ya mgawanyo wa kazi, kuwa nitamweleza mtu mhusika ambaye n iwewe ili ukiweza uwatembelee na tuone tunaweza kweli kuwasaidia vipi.
Mdau Geoffrey Ng'humba




0 comments:
Post a Comment