Nafasi Ya Matangazo

September 04, 2009

Wanakijiji walijitokeza katika mazishi ya mpendwa wetu Diana, hapa walikuwa wakijadili hili na lile. Kutoka Kushoto ni Mwalimu wangu wa English darasa la STD III, Mwal Mlay, Mfugaji Mzee Kisawani a.k.a Mrefu, Paul Ndee, Elihuruma Nyela, Joseph Msafiri na aliyetupa mgogo ni Mwalimu Mrutu. Kuwajia wanakijiji wenzako kwa majina kuna raha yake.
Mambo flani ya msosi uyalikuwepo na waandazi ndo mambo yalikuwa hivi.
Majonzi kwakweli... Bibi Diana a.k.a mama Mroki (kulia) akiwa katika majonzi mazito aliyemshika ni Mama Mkwe wa Father Kidevu, Mama Wiketye kutoka Mzumbe.
Faraja ilihitajika kila kona... Mama wa Marehemu Diana (katikati) akiwa na Wake wenzake, Mama Thomas (kushoto) na Mama Daniel. Waombolezaji wakiwa wamelibeba sanduku lililouhifadhi mwili wa Mpendwa wetu Diana.
Baba D...Onesmo akiwa amelalia Msalaba wa Binti yake huku Mchungaji Kiongozi wa KKKT Usharika wa Mzumbe, Mchungaji Tengeneza akiendesha ibada ya maziko.
Hapa ndipo ulipolala Mwili wa Mpendwa wetu Diana Onesmo. Diana alizaliwa tar 31/08/2008 na Kufariki Tar 01/09/2009 ikiwa ni baada ya kutimiza mwaka mmoja tu. Jina la Mungu lihimidiwe maana sisi tulimpenda na Mungu akampenda zaidi hata aakamua kumtwaa katika dunia hii.
Diana alizika Tarehe 02/09/2009, Katika Mtaa wa Mwanga, Kitongoji cha Kinyenze, Kijiji cha Kipera, Kata na Tarafa ya Mlali, Wilayani Mvomero mkoani Morogoro.
Posted by MROKI On Friday, September 04, 2009 5 comments

5 comments:

  1. Narudia tena, sikumfahamu Diana, ila nimeumia sana hasa baada ya hizi picha. Bwana ametoa na bwana ametwaa.,jina la bwana lihimidiwe. RIP Diana. Poleni wafiwa.

    ReplyDelete
  2. Pole Mroky.
    Mbona amefariki mdogo hivyo jamani? Kwani ilkuwaje? Aliugua au?

    ReplyDelete
  3. POLENI SANA NDIO KAZI YAMUNGU HIYO

    ReplyDelete
  4. Poleni sana kifo kimeniuma sana, bwana ametoa bwana ametwaa jina lake lihimidiwe!

    Says

    ReplyDelete
  5. Poleni sana kifo kimeniuma sana, bwana ametoa bwana ametwaa jina lake lihimidiwe!

    Says

    ReplyDelete

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo