Nafasi Ya Matangazo

March 08, 2026




Na Mwandishi wetu, Dodoma
Wanawake kutoka Tume ya Madini Makao Makuu pamoja na Ofisi ya Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Dodoma wameungana na wanawake wengine duniani kusherehekea maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, yaliyofanyika katika Shule ya Msingi Mbande, Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma.

Maadhimisho hayo yamewakutanisha wanawake kutoka taasisi mbalimbali za serikali na binafsi, yakilenga kuadhimisha mchango wa wanawake katika maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla.

Maadhimisho ya mwaka huu yanafanyika chini ya kauli mbiu isemayo: “Haki kwa wanawake na wasichana ni msingi wa maendeleo jumuishi kufikia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.”

Kauli mbiu hiyo inalenga kuhamasisha jamii kutambua umuhimu wa kuhakikisha wanawake na wasichana wanapata haki na fursa sawa katika elimu, uchumi na uongozi, hatua inayochangia kwa kiasi kikubwa katika kufanikisha maendeleo endelevu ya taifa.

Kupitia maadhimisho hayo, washiriki wamepata fursa ya kujadili namna ya kuendelea kuimarisha usawa wa kijinsia na kuhamasisha jamii kushiriki katika kuondoa vikwazo vinavyoweza kuzuia maendeleo ya wanawake na wasichana nchini.
Posted by MROKI On Sunday, March 08, 2026 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo