Nafasi Ya Matangazo

March 30, 2009

MWANDISHI wa Habari wa siku nyingi Hamidu Bisanga (59)amefariki dunia juzi kwa ajali ya gari iliyotokea katika eneo la Kijitonyama karibu na Millenium Tower.

Bisanga aliyezaliwa jijini Mwanza na kufanya kazi katika vyombo vya habari kama mwandishi na baadaye Meneja uhusiano sehemu mbalimbali nchini alifariki jumapili usiku.
Kwa mujibu wa Mke wa Marehemu Tunu Bisanga Mazishi ya mumewe yatafanyika leo saa 10 jioni katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.

Katika Uhai wake, Bisanga alifanya kazi kama Mhakiki wa lugha katika kiwanda cha Printpak mwaka 1973 hadi 1975 na baadaye katika Magazeti la Serikali ya SundayNews na DailyNews kuanzia mwaka 1975 hadi 1990 akiwa mwandishi wa habari na baadaye mwaka 1990 hadi 1994 alifanya kazi katika magazeti hayo akiwa Msanifu Mkuu.

Mwaka 1994 hadi 1998 aliajiriwa na Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) kama Afisa uhusiano na mwaka 1998 aliajiriwa na Shirika la Maendeleo (NDC) akiwa Meneja uhusiano hadi August mwaka jana alipohamia katika Kampuni ya BayPort kuwa Meneja Uhusiano na Masoko.

Pia Marehemu Bisanga aliishawahi kufanya kazi gazeti la The African, Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC),Sauti ya America na wakala wa Habari wa Ufaransa.

Msiba unafanyika nyumbani kwake Oysterbay mtaa wa Chisiza,ambapo marehemu ameacha mjane ,watoto watatu Ahmed,Khadija na Issa na mjukuu mmoja Alma.
Posted by MROKI On Monday, March 30, 2009 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo