Nafasi Ya Matangazo

February 15, 2009



Kibao cha Uzinduzi wa Uwanja mpya wa taifa
Rais Jakaya Kikwete na Mgeni wake Rais Hu Jintao wa China wakishangilia mara baada ya kuzindua kwa pamoja uwanja mpya wa taifa Dar es Salaam jana. Uwanja huu umejengwa ikiwa ni Juhudi za Rais wa Awamu ya tatu Benjamin Mkapa aliyowahidi watanzania kuwaachia baada ya utawala wake. Serikali za China na Tanzania zilishirikiana katika ujenzi wake. Pia uwanja wa zamani wa taifa umebadilishwa jina na ssa utaitwa Uwanja wa Uhuru a.k.a Shamba la bibi.
Viongozi wa Serikali toka kushoto ni Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais, Dk. Ali Mohamed Shein, Waziri Mkuu , Mizengo Pinda na rais Mstaafu Benja Mini Mkapa ambaye alitoa wazo la ujenzi wa uwanja huo.Rais Hu Juntao wa China akisalimiana na wasanii wa Taasisi ya Sanaa Bagamoyo waliokuwa wakitumbuiza wakati wa sherehe za uzinduzi wa Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.



Kundi la Ngoma la JKT likitumbuiza uwanjani hapo.
Wasanii wa Taasisi ya Sanaa Bagamoyo wakitumbuiza kwa michezo ya Kichina. Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa na makamu wa Rais Dk. Ali Mohamed Shein wakiingia katika uwanja huo mpya huku Mkapa akistaajabu madhari ya uwanja huo.
Posted by MROKI On Sunday, February 15, 2009 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo