Nafasi Ya Matangazo

February 14, 2009

Na Mroki Mroki-
JUMANNE wiki hii Rais Jakaya Kikwete na Naohodha Mkuu wa Michezo nchini, aliialika timu ya Tiafa “Taifa Stars” Ikulu Dar es Salaam kwaajili ya kula nao chakula cha mchana.

Binafsi naupongeza uamuzi huo wa kiongozi wa juu wan chi kuialika timu kwaajili yam lo wa mchana, ni moja ya hamasa kwa wacchezaji wetu ambao wanajukumu kubwa mbele yao katika fainali za Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) nchini Ivory Coast.

Nakumbuka Rais katika salamu zake kabla ya kuanza kula, maana na mimi nilikuwa mmoja wa Mwandishi Mpigapicha niliyebahatika katika mwaliko huo Ikulu, Rais alisema adhma yake hiyo ilikuwa aifanye tangu timu iliporejea toka Sudan ilipofuzu fainali hizo za CHAN.

Sitaki kuzungumzia utamu wa chakula hicho hapa maana naimani nitakuwa natoa mateso na kujaza vinywa vya wengi mate pasipo sababu, ndio si mnajua maanjumati ya ‘State’yalivyo.

Mimi nitazungumzia mambo mawili yaliyonikera na hakika wengi wenu hata wewe msomaji lilikukera ila tu huna pa kulisemea, mimi nitalisema kwa niaba yako.

Mambo haya ni mavazi ya timu yetu unapoingia katika sehemu nyeti ya nchi kama Ikulu na nidhamu ya mchezaji moja moja mbele ya kiongozi wa nchi.

Ikulu kwa maneno ya Hayati baba wa taifa Julius Nyerere hala patakatifu” panapohitajhi nidhamu na heshima ya hali yajuu.

Iweje leo timu ya taifa inaalikwa Ikulu, kula chakula cha mchana na Rais halafu mnavaa fulana na chini kila mmoja na kiatu rangi tofauti? Lazima tuwe tofauti tangu sasa.

Kuna tatizo gani na fedha zote za udhamini zinazomwaga kila mchezaji akawa na suti maalum ya kusafiria na katika mialiko mikubwa kama ya Rais na Bungeni.

Siku ile ilikuwa ni aibu maan Rais alikuwa nja ugeni mkubwa sana wa Rais wa Zambia na muda timu ya taifa inaingia Ikulu Rais huyo alikuwapo kwaajili ya kuaga.

Mathalani Rais Kikwete akisema amuonyeshe mwenzake anavyopenda timu yake kuwa “ Banda, hawa vijana wangu wa timu ya Taifa , ntakula nao chakula cha mchana leo’ Kha! Rais Rupiah Banda angestaajabu kuona vijana wapo katika vazi la ajabu na sio suti nadhifu.

Haya hizo suti za michezo zenyewe walizovaa wengine walizikunja chini kama wanaenda kuruka maji. Aibu sana hii kwa taifa na Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) ambao ndio wasimamizi wa timu.

Jambo la pili ni nidhamu ya wachezaji wakati wa kusalimiana na Rais, haiwezekani leo unapeana mkono na Rais halafu unaweka mikono mfukoni kana kwamba huyo ni sawa yako.

Ninakataa kabisa jambo hili na nasema ukweli wachezaji wetu lazima tubadilike na siku nyingine ikitokea hivi basi tuwaambie wazazi wetu hatuendi hatuna nguo.

Nakumbuka hata baada ya kuishinda Burkinafaso Bunge liliwapa heshima na kuwaalika Bungeni na kuvinja kanuni za Bunge kwa wachezaji hao kukanyaga zulia la Bunge na sutizao za michezo.

Mbona Wabunge wenyewe hawaruhusiwi kukanyaga zulia lile hata wakiwa wamevaa shati na tai? Nasema waliwastahi tu lakini msingeingia mimi ningekuwa Spika.

Viongozi wa michezo na vilabu na hata TFF tuhakikishe tunakuwashonea mavazi ya heshima wachezaji wetu kwaajili ya dhifa na mialiko mikubwa kama hiyo pamoja na safari za nje, tuwaige wenzetu.

Na tukemee nidhamu zisizokuwa na utamaduni wetu, na siku tyukisafiri kwenda katika Fainali za CHAN huko Ivory Coast tupige vitu na kuonyesha mataifa mengine kuwa nchi yetu rais anapenda soka na timu yetu kweli ni JK Boys.

NB: HAYA NI MAONI YA UICHAMBUZI WA GAZETI LA HABARILEO, FEBRUARI 14 2009.
Nini Maoni yenu wadau.
Posted by MROKI On Saturday, February 14, 2009 2 comments

2 comments:

  1. BABA KIDEVU HAPO NIMEKUPATA HASA, WALE WACHZAJI WALINIUDHI KUFA, NILITAMANI NIWE MAXIMO NIWACHARAZE VIBOKO.WAKATI RAISI ALIWASALIMIA KWA MIKONO MIWILI WAO WALITIA KINYAA,MKONO MMOJA TENA KWA SURA ZA KUTOJARI KABISA, MAVAZI YALIUMIZA KICHWA MBAYA,UTAFIKIR WALITAKA KWENDA MIKADI KUOGELEA.
    TATIZO LAKINI NI ELIMU, WOTE WAMEOKOTWA MITAANI NA HAKUNA SHULE KABISA, SASA HIYO NIDHAMU WAPI.
    LAWAMA PIA KWA KOCHA NA VIONGOZI WA TFF, WANASTAHILI KUWASHEPU WACHEZAJI WAO.
    WANATIA AIBU SANA. NASHUKURU MLOKO LABDA WAMESIKIA, LABDA WATABADIRIKA.

    ReplyDelete
  2. Mkuu Mroki na Mdau hapo juu, Msemayo ni kweli kabisa, wachezaji wetu wa timu ya Taifa wanatakiwa kupikwa kinidhamu.Na ni kweli suala la elimu pia linachangia, lakini pia lawana lazima ziende zaidi kwa TFF naona katika suala hili wamejisahau kidogo. Walitakiwa wawape kadarasa ka muda mchache "how to behave" kwa sababu ile ni sehemu nyingine tofauti na uwanjani au kambini. kwani hawakumuona jinsi maximo alivyokuwa kwa heshima na kuonyesha unyenyekevu(ukitizama picha zilizopigwa). Kuhusu mavazi nadhani ni kuzembea tu, maana nakumbuka miaka ya nyuma timu za taifa iwe ya mchezo wowote ule walikuwa wanavaa suti wasafiripo kwenda nje ya nchi kwenye mashindano, hata kwenye sherehe za ufunguzi. Chama ambacho naona kime -maintain ustaarabu huo ni chama cha riadha na TOC kwa miaka ya hivi karibuni, ingawa mwaka jana TOC nao walichemsha kwenye sherehe za ufunguzi za Olympics, Beijing.Vyama vyetu na mashirikisho ya michezo mbalimbali zina uongozi wenye viongozi kibao, sasa kazi yao wengine hapo ni nini kama sio pamoja na kufundisha na kujenga maadili ya mwanamichezo hasa inapokuja katika uwakilishi wa taifa?!!!Hata katika Vilabu pia inapokuja suala la kuiwakilisha nchi Vyama vya michezo taifa lazima vichukue jukumu hilo, Kwani wale viongozi wanaoandamana na timu huwa wa nini?. Tuamke sasa wasidhani watu wanalaumu bure, leo wachezaji hawa wamealikwa Ikulu kwa JK,ni aibu yetu tumeificha humuhumu ndani kwetu, kesho wakikutana na Raisi mwingine si aibu tupu!!?

    ReplyDelete

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo