Mpigapicha wa gazeti la Habari Leo linalomilikiwa na serikali Mroki Mroki akipigwa na polisi mwenye namba D9346 (kulia) wa kituo cha polisi Oysetrbay jijini Dar es Salaam katika mahafali ya 20 ya Chuo Kikuu Huria yaliyofanyika Oktoba 26 2008.
Je sheria inasemaje hapa...
Pole Mrocky kumbe ulipigwa ndo mana ulikuwa hu apdeti picha humu kumbe ulikuwa unauguza majeraha!
ReplyDeletePole sana. Maana mi nilikuwa nashangaa, kila nikifungua picha ni zile zile za Bathdei ya Kikwete, ikawa asubuhi ikawa jioni, mpaka nikamuuliza Mjengwa bwana.
Karibu tena na pole
Kazi Ipo:-(
ReplyDeleteMimi napenda kuuliza, je, katika hali kama hii polisi nae akikung'utwa ngumi ni kosa? Kwakuwa nafahamu matendo yote ya kupiga mtu au watu kupigana ni kinyume cha sheria za nchi.Tena jambo hili likitendeka hadharani ni mbaya zaidi Je, hawa polisi wanapata wapi haki hii?
ReplyDeleteWanatumia kisingizio cha kutuliza ghasia sasa kama kuna hali ya "ghasia" mbona wao wanakuwa salama?
Kujichukulia sheria mkononi kwa hawa mapolisi ndo kumemfikisha ZOMBE hapo alipo. Pole mroki
Pole Mrocky naona afande ame-connect lakini yaonekana pia umejaribu kuikwepa. Hiyo ndiyo adha ya uandishi mjomba.
ReplyDeletepole sana mabadiliko yataletwa na sisi wenyewe wananchi. Hao askari lazima wachukuliwe hatua za kisheria ikibidi jeshi la polisi kukulipia matibabu na huyo askari kuwajibishwa kama mfano kwa wanausalama wengine nchini.
ReplyDeleteNdugu zetu hawa Polisi, wakati mwingine ni watu wa kusamehe tuuu. Wengi wanaishi maisha magumu sana. Nenda Pale ukonga FFU uone wanavyoishi, hii inachangia sana kwa wao kuwa hasira za ajabu. Maisha wanayoishi ni sawa kama wamerogwa wengi wao wako psycological affected. Hata huyu hajui kama pale alivunja sheria ya nchi ingawa yy ni askari. Ple mroky
ReplyDelete