Nafasi Ya Matangazo

March 20, 2016

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, akitoa hotuba ya uzinduzi wa msimu wa mashindano ya Miss Tanzania 2016 kwenye hoteli ya Ramada Kunduchi jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia Machi 20, 2016. 
 Waziri akiwa katika picha ya pamoja na Kaamti ya Miss Tanzania, na Katibu Mtendaji wa Basata, Mwita Gesimba
 Waziri akifurahia wakati wa uzinduzi huo
 Miss Tanzania anayemaliza muda wake, Lilian Kamazima, (mwenye taji), akiwa katika picha ya pamoja na watangulizi wake. 
 *********
NA K-VIS MEDIA.Khalfan Said
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, amezindua rasmi msimu wa mashindano ya kumtafuta mlimbwende yaani Miss Tanzania kwa mwaka huu wa 2016.

Katika hotuba yake, Nape amesema serikali imebariki mashindano hayo kwani ni moja ya njia za kukuza vipaji na kuongeza ajira, na kisha akatania, “Ninawatakia kila la heri Miss World wa mwaka huu atoke Tanzania, na tena mkitaka kujua mbinu za ushindi mnitafute niwafundishe bao la mkono.” Alisema waziri Nape na kusababisha hadhira kuangua kicheko.

Uzinduzi huo uliofanyika usiku wa kuamkia leo Machi 20, kwenye ukumbi wa Hoteli ya Ramada iliyoko Kunduchi jijini Dar es Salaam, ulihudhuriwa na wadau mbalimbali wa tasnia ya urembo, wakiwemo waliowahi kuwa warembo wa shindano hilo la Miss Tanzania miaka iliyopita.

Pia Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa, Mwita Gesimba, alihudhuria hafla hiyo iliyopambwa na wasanii, Wanne Star, na Lina.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Lino International Agency Limited, ambao ndio waandaaji wa shindano hilo, Hashim Lundenga, mashindano ya mwaka huu yamebeba kauli mbiu ya mwaka huu ni “Mrembo na Mazingira”, nah ii ni kuonyesha mchango wa tasnia hii katika kuhamasisha umma kutunza mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Tayari Mamlaka ya Utabiri wa Hali ya Hewa Nchini, (TMA), imetoa tahadhari kwa wwakazi wa miji ya Dar es Salaam na Moshi, kuwa leo hii huenda pakawa na joto ambalo halijawahi kushuhudiwa nchini na kuwataka wananchi watulie majumbani labda wale wenye mahitaji muhimu sana.

TMA inasema joto kwa jiji la Dar es Salaam litapanda hadi nyuzi joto 35 wakati kule Kilimanjaro litapanda hadi kufikia nyuzi joto 36.

Watu wametakiwa kunywa maji kwa wingi ili kukabiliana na hali hiyo
 Waziri Nape akizungumza na Hashim Lundenga, (kulia)
 Msanii wa Bongo Flava, Lina akiimba kwa hisia
 Waziri akipewa "Breafing" maelezo kwa kifupi kuhusu tukio hilo, muda mfupi baada ya kuwasili 
Wadau

Wadau
 Katibu Mkuu wa Kamati ya Miss Tanzania, Bosco Majaliwa, (kulia) na baadhi ya wajumbe na wadau
 Miss Tanzania anayemaliza muda wake, Lilian Kamazima akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa kamati
 Kikundi cha Wanne Star
 Lundenga akitoa hotuba, (kulia) ni Lilian
 Waziri Nape, akisalimiana na mmoja wa wajumbe wa kamati ya Miss Tanzania, Almish Hazal
 Hoyce Temu, (katikati), akizungumza wakati wa Breafing na waziri
Burudani ikiendelea
Posted by MROKI On Sunday, March 20, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo