Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, akitoa hotuba ya uzinduzi wa msimu wa mashindano
ya Miss Tanzania 2016 kwenye hoteli ya Ramada Kunduchi jijini Dar es Salaam,
usiku wa kuamkia Machi 20, 2016.
Waziri akiwa katika picha ya pamoja na Kaamti ya Miss Tanzania, na Katibu Mtendaji wa Basata, Mwita Gesimba
Waziri akifurahia wakati wa uzinduzi huo
Miss Tanzania anayemaliza muda wake, Lilian Kamazima, (mwenye taji), akiwa katika picha ya pamoja na watangulizi wake.
*********
NA K-VIS MEDIA.Khalfan Said
WAZIRI wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, amezindua rasmi msimu wa mashindano ya kumtafuta
mlimbwende yaani Miss Tanzania kwa mwaka huu wa 2016.
Katika hotuba yake, Nape
amesema serikali imebariki mashindano hayo kwani ni moja ya njia za kukuza
vipaji na kuongeza ajira, na kisha akatania, “Ninawatakia kila la heri Miss
World wa mwaka huu atoke Tanzania, na tena mkitaka kujua mbinu za ushindi
mnitafute niwafundishe bao la mkono.” Alisema waziri Nape na kusababisha
hadhira kuangua kicheko.
Uzinduzi huo uliofanyika usiku
wa kuamkia leo Machi 20, kwenye ukumbi wa Hoteli ya Ramada iliyoko Kunduchi
jijini Dar es Salaam, ulihudhuriwa na wadau mbalimbali wa tasnia ya urembo,
wakiwemo waliowahi kuwa warembo wa shindano hilo la Miss Tanzania miaka
iliyopita.
Pia Katibu Mtendaji wa Baraza
la Sanaa la Taifa, Mwita Gesimba, alihudhuria hafla hiyo iliyopambwa na
wasanii, Wanne Star, na Lina.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa
Lino International Agency Limited, ambao ndio waandaaji wa shindano hilo,
Hashim Lundenga, mashindano ya mwaka huu yamebeba kauli mbiu ya mwaka huu ni
“Mrembo na Mazingira”, nah ii ni kuonyesha mchango wa tasnia hii katika
kuhamasisha umma kutunza mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Tayari Mamlaka ya Utabiri wa
Hali ya Hewa Nchini, (TMA), imetoa tahadhari kwa wwakazi wa miji ya Dar es
Salaam na Moshi, kuwa leo hii huenda pakawa na joto ambalo halijawahi
kushuhudiwa nchini na kuwataka wananchi watulie majumbani labda wale wenye
mahitaji muhimu sana.
TMA inasema joto kwa jiji la
Dar es Salaam litapanda hadi nyuzi joto 35 wakati kule Kilimanjaro litapanda
hadi kufikia nyuzi joto 36.
Watu wametakiwa kunywa maji kwa
wingi ili kukabiliana na hali hiyo
Waziri Nape akizungumza na Hashim Lundenga, (kulia)
Msanii wa Bongo Flava, Lina akiimba kwa hisia
Waziri akipewa "Breafing" maelezo kwa kifupi kuhusu tukio hilo, muda mfupi baada ya kuwasili
Wadau |
Wadau
Katibu Mkuu wa Kamati ya Miss Tanzania, Bosco Majaliwa, (kulia) na baadhi ya wajumbe na wadau
Miss Tanzania anayemaliza muda wake, Lilian Kamazima akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa kamati
Kikundi cha Wanne Star
Lundenga akitoa hotuba, (kulia) ni Lilian
Waziri Nape, akisalimiana na mmoja wa wajumbe wa kamati ya Miss Tanzania, Almish Hazal
Hoyce Temu, (katikati), akizungumza wakati wa Breafing na waziri
Burudani ikiendelea
0 comments:
Post a Comment