SHIRIKA la Majisafi na Majitaka jijini Dar es
Salaam (DAWASCO) limewapiga faini ya shilingi milioni 17 raia wa China
wanaofanya kazi kwenye wizara ya afya (Chinese medical team) baada yakubaini
wizi mkubwa wa maji kwenye nyumba wanayoishi iliyopo mtaa wa Mtwara Oysterbay
Jijini Dar es salaam.
Akizungumza kwenye eneo la tukio Meneja wa Dawasco
Kinondoni, Judith Singinika alisema waliwabaini wizi huo baada ya kufanya operesheni
maalum kwenye mtaa huo ya kubaini wizi wa maji ndipo walipofanikiwa kunasa nyumba
hiyo ikiwa imeunganishiwa maji pasipo mita na kukuta imefungwa pampu kubwa ya
kuvuta maji kutoka kwenye laini ya bomba kubwa.
“Dawasco tumewapiga faini raia wa China kiasi cha
shilingi milioni 17 baada yakuwanasa wamejiunganishia huduma ya maji kinyume na
utaratibu na laini inayopeleka maji ndani haina mita na imefungwa pampu kubwa
yakuvuta maji wakati sio utaratibu hivyo tumeng’oa pampu na nakuwapiga faini,”alisema
Singinika.
Singinika alisema raia hao wa china watalazimika
kulipa fedha hizo ndani ya miezi 24 ambapo kila mwezi watalipa sh laki saba kwa
dawasco.
Meneja huyo wa Dawasco amesisitiza kuwa operesheni
hiyo yakukamata wezi wa maji kwenye maeneo tofauti ya ijini Dar es Salaam
niendelevu na inatokana na agizo la Waziri wa maji na umwagiliaji, Gerson
Lwenge ambapo alilitaka shirika hilo kukagua majengo yote makubwa pamoja na
viwanda nakujiridhisha matumizi yake ya maji.
Dawasco inaendelea kuwasihi watu wote
waliojiunganishia huduma ya Maji kiholela kinyume cha utaratibu kwenye nyumba
za makazi, majengo makubwa pamoja na viwanda kujisalimisha nakutambuliwa kwani
hatua kali za kisheria zitachukuliwa endapo wakibainika kwani ndio
wanaolikosesha Shirika mapato.
0 comments:
Post a Comment