Nafasi Ya Matangazo

February 02, 2014

Mshambuliaji machachari wa timu ya Yanga,Mrisho Ngassa (17) akichuana vikali kuwania mpira na Beki wa Timu ya Mbeya City,Deogratias Julius wakati wa mtanange wa Ligi kuu Tanzania Bara uliomalizika hivi sasa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Dakika 90 za mchezo zimemalizika hivi punde na Yanga imeshinda kwa Bao 1-0 lililotiwa kimiani na Mrisho Ngassa,dakika ya 15 ya mchezo kipindi cha kwanza.
*********
Mshambuliaji wa Yanga ya Dar es Salaam Mrisho Khalfan Ngassa leo amefanikiwa kuipatia timu yake ya kwanza pointi 3 muhimu baada ya bao lake pekee kuizamisha timu ngumu ya jiji la Mbeya, Mbeya City ndani ya uwanja wa taifa.

Kwa matokeo hayo Yanga sasa imevunja ugumu wa kutokufungwa hata mcezo mmoja kwa timu hiyo ya  Mbeya ambayo imekuwa ikifanya vyema na kuzikamia timu zote za ligi kuu ya soka Tanzania bara.

Licha ya matokeo hayo Yanga imebaki nafasi ya pili baada ya Azam FC nayo kuifunga Kagera Suger 4-0 na kufikisha point 36 na Yanga kubaki na pointi 35.33 na Mbeya City ikibaki nafasi ya 3 na pointi 31 huku Simba ikiwa nafasi ya nne kwa pointi 30 lakini ikiwa na mchezo mmoja mkononi.
 Beki wa Timu ya Mbeya City,Deogratias Julius akijiandaa kuondosha hatari iliyokuwa imekwenda langoni kwao.

Kiungo mshambuliaji wa Yanga,Haroun Niyonzima  pamoja na Beki wa Mbeya City,Yussuf Abdallah wakiwania mpira,wakati wa mchezo wao wa marudiano katika mzungunguko wa pili wa Ligi kuu Tanzania Bara uliomalizika hivi sasa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
 Mashabiki wa Mbeya City wakiendelea kuishangilia timu yao.

























































































































































Posted by MROKI On Sunday, February 02, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo