Mshambuliaji
machachari wa timu ya Yanga,Mrisho Ngassa (17) akichuana vikali kuwania
mpira na Beki wa Timu ya Mbeya City,Deogratias Julius wakati wa
mtanange wa Ligi kuu Tanzania Bara uliomalizika hivi sasa kwenye Uwanja
wa Taifa jijini Dar es Salaam.Dakika 90 za mchezo zimemalizika hivi
punde na Yanga imeshinda kwa Bao 1-0 lililotiwa kimiani na Mrisho
Ngassa,dakika ya 15 ya mchezo kipindi cha kwanza.
Mshambuliaji
wa Yanga ya Dar es Salaam Mrisho Khalfan Ngassa leo amefanikiwa
kuipatia timu yake ya kwanza pointi 3 muhimu baada ya bao lake pekee
kuizamisha timu ngumu ya jiji la Mbeya, Mbeya City ndani ya uwanja wa
taifa.
Kwa
matokeo hayo Yanga sasa imevunja ugumu wa kutokufungwa hata mcezo mmoja
kwa timu hiyo ya Mbeya ambayo imekuwa ikifanya vyema na kuzikamia timu
zote za ligi kuu ya soka Tanzania bara.
Licha ya matokeo hayo Yanga imebaki nafasi ya pili baada ya Azam FC nayo kuifunga Kagera Suger 4-0 na kufikisha point 36
na Yanga kubaki na pointi 35.33 na Mbeya City ikibaki nafasi ya
3 na pointi 31 huku Simba ikiwa nafasi ya nne kwa pointi 30 lakini
ikiwa na mchezo mmoja mkononi.
Beki wa Timu ya Mbeya City,Deogratias Julius akijiandaa kuondosha hatari iliyokuwa imekwenda langoni kwao.
Kiungo mshambuliaji wa Yanga,Haroun Niyonzima pamoja na Beki wa Mbeya City,Yussuf Abdallah wakiwania mpira,wakati wa
mchezo wao wa marudiano katika mzungunguko wa pili wa Ligi kuu Tanzania
Bara uliomalizika hivi sasa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es
Salaam.
Mashabiki wa Mbeya City wakiendelea kuishangilia timu yao.
|
0 comments:
Post a Comment