Nafasi Ya Matangazo

May 08, 2010

Mpigapicha wa gazeti HABARILEO, Athumani Hamisi (kwenyekiti) alirejea nyumbani Dar es Salaam leo akitokea nchini Afrika Kusini alikwenda Septemba 28, 2008 kwa matibabu kufuatia ajali ya gari aliyoipata Septemba 12 mwaka huo akiwa njiani kwenda Kilwa mkoani Lindi kikazi. Kushoto aliyeshika shada la maua ni muuguzi kutoka Afrika Kusini aliyemsindikiza.
Mwenyekiti wa Chama cha Wapigapicha za Habari Tanzania (PPAT) Mwanzo Milinga akimpa mkono Athumani baada ya kuwasili.
Baba Mzazi wa Athumani, Mzee Hamisi Msengi akimsalimia mwanae
Ndugu jamaa na marafiki wakiwa na Athumani
Wanachama na viongozi wa PPAT wakimsalimia Athumani.
Naibu Mhariri wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali TSN, Mkubwa Ally (kulia) na Matina Nkuru kutoka Vodacom wakimsalimia Athumani.
Katibu Mtendaji wa PPAT, na Mpigapicha wa Magazeti ya serikali ya Daily News, Sunday News, HABARILEO na HABARILEO Jumapili na Mwendeshaji wa libeneke hili Mroki Mroki 'Father Kidevu' (kulia) akimsalimia Athumani ambaye ni mkuu wake wa Kitengo cha Picha HABARILEO.
Debora Mroki nae alikuwepo uwanjani hapo kumpokea Shemeji yake.
Athumani akipakia katika gari maalum la wagonjwa kupelekwa nyumbani kwake Sinza Dar es Salaam.
HII ILIKUWA 28/09/2008 akipelekwa Afrika Kusini Athumani aliumia zaidi kifua na shingo alisafirishwa jana kwa ndege ya ATCL.Blog hii inamuombea kwa Mungu amjalie afya njema haraka na matibabu mema.
Hili ndo gari alilopatanalo Ajali Athumani siku akienda Kilwa mkoani Lindi kikazi. Ilikuwa 12/09/2008.
Posted by MROKI On Saturday, May 08, 2010 2 comments

2 comments:

  1. AnonymousMay 09, 2010

    vp hana mke?mbona hamjapiga picha mkewe akimpokea mume wake.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 12, 2010

    pole sana kaka yangu nimejisikia vibaya sana nilivyomuona kama athuman katika picha hizi na jinsi alivyo imeniumiza sana namwombea mwenyezi mungu amsaidia na amponyeshe kabisa jamani hivyo ashukurukiwe mungu jinsi hali ya gari ilivyo na kuona hadi leo anapumua ni rehemu za mola, ila kaka hamis si alioa mwandishi mwenzake na alizaa nae mbona sijamuona hapo? huo ni ubaguzi jamani mke wala mtoto si busara wapiga picha

    ReplyDelete

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo