Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, amemtembelea na kumpa pole Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Nkasi, Mhe. Ally Mohamed Keissy, kufuatia msiba wa shimeji yake - dada wa mkewe uliotokea hivi karibuni.
Dkt Kikwete akioneshwa nyumba aliyowahi kushi akiwa afisa wa CCM miaka ya 1980 alipomtembelea na kumpa pole Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Nkasi, Mhe. Ally Mohamed Keissy, kufuatia msiba wa shimeji yake - dada wa mkewe uliotokea hivi karibuni.
*************
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, amemtembelea na kumpa pole Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Nkasi, Mhe. Ally Mohamed Keissy, kufuatia msiba wa shimeji yake - dada wa mkewe uliotokea hivi karibuni.Dkt Kikwete alimtembelea Mhe. Keissy nyumbani kwake katika eneo la Cheyo, mjini Tabora, tarehe 14 Septemba 2026, muda mfupi baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi ya siku nne mkoani Tabora.
Ziara hiyo ya kutoa pole ilikuwa pia na kumbukumbu ya pekee kwa Dkt Kikwete, kwani eneo la Cheyo si geni kwake. Yeye mwenyewe liwahi kuishi katika eneo hilo na jirani na nyumba ya Mhe. Keissy miaka ya 1980 alipokuwa akifanya kazi mkoani Tabora akiwa Afisa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Katika ziara hiyo, Dkt Kikwete aliambatana na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Dkt Jafaar Seif, pamoja na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Upendo Wella, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Tabora.
Dkt Kikwete alimpa Mhe. Keissy na familia yake pole kwa msiba huo na kuwatakia moyo wa subira na faraja katika kipindi hiki cha majonzi.










0 comments:
Post a Comment