Nafasi Ya Matangazo

August 02, 2026

 



Dodoma
Waziri wa Kilimo Mhe.Daniel Chongolo (Mb) leo tarehe 02 Agosti 2026,ameongoza mamia ya washiriki katika Marathon ya Maadhimisho ya Miaka 10 ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) Katika Viwanja vya Dkt.Samweli Malecela Nane Nane Nzuguni jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka kumi tangu kuanzishwa kwa taasisi hiyo.

Marathon hiyo imewakutanisha viongozi wa serikali, watafiti, wadau wa sekta ya kilimo, wanamichezo pamoja na wananchi kutoka maeneo mbalimbali nchini, kwa lengo la kuhamasisha Utafiti kwa usalama wa chakula DIRA 2050, kuboresha afya, mshikamano na kutambua mchango wa TARI katika kuendeleza tafiti na teknolojia zinazochochea maendeleo ya sekta ya kilimo nchini.

Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa mbio hizo, Waziri wa Kilimo amesema katika kipindi cha miaka 10, TARI imeendelea kuwa nguzo muhimu katika kuibua ubunifu na kufanya tafiti zilizochangia kuongeza tija ya uzalishaji, kuimarisha usalama wa chakula na kuinua uchumi wa wakulima nchini.

Aidha, ametoa wito kwa wananchi kuendelea kuunga mkono tafiti za kilimo na matumizi ya teknolojia zinazozalishwa na TARI ili kuongeza uzalishaji na kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya kilimo.

Maadhimisho ya Miaka 10 ya TARI yanatarajiwa kuendelea kwa shughuli mbalimbali zikiwemo maonesho ya teknolojia za kilimo, elimu kwa wananchi na utoaji wa huduma za ushauri wa kitaalamu kwa wadau wa sekta hiyo.

TARI ilianzishwa kwa Sheria Na. 10 ya Mwaka 2016








Posted by MROKI On Sunday, August 02, 2026 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo