Nafasi Ya Matangazo

August 10, 2026



Kuelekea Maadhimisho ya miaka 20 ya Polisi Jamii nchini, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limewataka Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Lyoto kutoa taarifa za uhalifu.

Wito huo umetolewa Agosti 10, 2026 na Polisi Kata ya Ilemi Mkaguzi wa Polisi Elibariki Mambuye wakati akizungumza na Walimu na Wanafunzi hao na kuwahimiza kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za uhalifu ili kuzuia vitendo hivyo katika jamii.

Aidha, Mkaguzi wa Polisi Mambuye amewaeleza Walimu na Wanafunzi wa Shule hiyo kuhusu Maadhimisho ya miaka 20 ya Polisi Jamii ambayo yatafanyika kitaifa Mkoani Mbeya yakiwa yamebeba kauli mbiu inayosema, Miaka 20 ya Polisi Jamii: Tushirikiane kuimarisha Amani, Usalama na Umoja wa Kitaifa.
Posted by MROKI On Monday, August 10, 2026 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo