Nafasi Ya Matangazo

August 02, 2026

Maandalizi ya Kizimkazi Festival itakayofanyika Agosti 12 hadi 14, 2026, yamepamba moto. Tamasha hili linalofanyika kila mwaka linatayarajiwa kuwaleta pamoja wananchi, wadau wa utalii, biashara, burudani na uchumi wa buluu katika mandhari ya kipekee ya Kizimkazi visiwani Zanzibar.


Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa  Kamati ya Maandalizi ya Tamasha, Mahfoudh Said Omar, shamrashamra zitaanza Agosti 12 kwa matembezi ya pamoja, yakifuatiwa na maonyesho ya biashara, mdahalo wa uchumi wa buluu na mashindano ya ngalawa yatakayopamba mwambao wa Bahari ya Hindi.

Agosti 13 kutakuwa na uzinduzi wa miradi ya maendeleo na mdahalo wa Nishati Safi, na kisha usiku wake kutakua na tamasha kubnwa la muziki lijulikanalo kama ‘Usiku wa Kizimkazi’ litakalowakutanisha wasanii wakubwa nchini, na maelfu ya wananchi kwa burudani ya pamoja.

Kilele cha Tamasha hilo kitakua Agosti 14 kwa kusherehekewa urithi wa Kizimkazi, vivutio vya utalii na fursa mbalimbali za maendeleo zinazofungua milan
Posted by MROKI On Sunday, August 02, 2026 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo