Mhe. Dkt. Evaline Wilbard Munisi akila kiapo kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi Ajira na Mahusiano) iliyofanyika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma, tarehe 06 Mei, 2026.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Mhe. Dkt. Evaline Wilbard Munisi kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya
Waziri Mkuu (Kazi Ajira na Mahusiano) kwenye hafla iliyofanyika Ikulu ya
Chamwino mkoani Dodoma, tarehe 06 Mei, 2026.
Rais Dkt. Samia amesema uteuzi wa Dkt. Munisi, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa NCCRMageuzi, umetokana na sifa, uwezo na uzoefu wake katika masuala ya umma na mahusiano, akisema Watanzania wote wana wajibu wa kuunganisha nguvu katika kulitumikia Taifa bila kujali tofauti za itikadi za vyama.
“Evaline ni Katibu Mkuu wa chama cha upinzani cha NCCR-Mageuzi; lakini nimeangalia wasifu wake, nikaona ana sifa za kuingia ndani ya Serikali na kutusaidia,” amesema Rais Dkt. Samia.
Halikadhalika, amemtaka Dkt. Munisi kushirikiana na viongozi na watendaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira na Mahusiano kusimamia kazi zenye staha, haki na stahiki za wafanyakazi katika sekta ya umma na binafsi, pamoja na juhudi za kutafuta na kulinda fursa za ajira kwa vijana wa Tanzania nje ya nchi.
Amesema Ofisi hiyo pia ina jukumu la kuimarisha mahusiano kati ya Serikali, waajiri na waajiriwa, pamoja na mahusiano ya kuheshimiana baina ya Serikali na mihimili mbalimbali ya dola.
Kwa upande wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA), Rais Dkt. Samia amemtaka Mtendaji Mkuu Dkt. Kheri Mahimbali kusimamia vyema taasisi hiyo ili kurejesha ufanisi na imani yake kwa umma, hususan baada ya hoja na changamoto zilizoibuliwa katika ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Rais Dkt. Samia amewataka viongozi hao kutekeleza majukumu yao kwa nidhamu, unyenyekevu na matokeo, akisisitiza kuwa dhamana ya uongozi inapaswa kuelekezwa katika kutatua changamoto za wananchi.
“Vyeo ni dhamana. Mungu amekuweka hapo ili utumikie watu,” amesema Rais Dkt. Samia.
Viongozi wengine walioapa kiapo cha uadilifu kwa watumishi wa umma ni: Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Ndugu Kheri Abdul Mahimbali;
Katibu wa Rais, Balozi Ali Jabir Mwadini; Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano
Tanzania (TCRA), Mhandisi Peter Philip Mwasalyanda; Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka
ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Dkt. Jabir Kuwe Bakari; na Mshauri wa Rais,
Masuala ya Jamii, Mhe. Angela Charles Kizigha (Mb.)
Viongozi mbalimbali wakiapa kiapo cha Maadili
kwenye hafla iliyofanyika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma tarehe 06 Mei, 2026.
Kutoka kulia ni; Ndugu Kheri Abdul Mahimbali Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Balozi Ali Jabir Mwadini, Katibu wa Rais, Mhandisi Peter Phillip Mwasalyanda Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Jabir Kuwe Bakari Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Mhe.
Angela Charles Kizigha, Mshauri wa Rais, Masuala ya Jamii

Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye hafla ya
Uapisho wa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi Ajira na Mahusiano)
Mhe. Dkt. Evaline Wilbard Munisi, Ikulu Chamwino
mkoani Dodoma tarehe 06 Mei, 2026.

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na
Viongozi mbalimbali mara baada ya kumuapisha Naibu Waziri, Ofisi ya
Waziri Mkuu (Kazi Ajira na Mahusiano) Mhe. Dkt.
Evaline Wilbard Munisi, Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 06
Mei, 2026.

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri Mkuu Mhe. Dkt.
Mwigulu Nchemba, Spika wa Bunge Mhe. Mussa Azzan Zungu, Katibu Mkuu Kiongozi
Mhe. Balozi Dkt. Moses Kusiluka, Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji Sivangilwa
Mwangesi katika picha na Naibu
Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi Ajira na Mahusiano) Dkt.
Evaline Wilbard Munisi, Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma tarehe 06
Mei, 2026.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Naibu Waziri, Ofisi ya
Waziri Mkuu (Kazi Ajira na Mahusiano) Dkt. Evaline Wilbard Munisi, Ikulu ya Chamwino
mkoani Dodoma tarehe 06 Mei, 2026.

0 comments:
Post a Comment