Nafasi Ya Matangazo

September 21, 2025

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mvomero kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Sara Msafiri Ally, akipiga goti la heshima na unyenuekevu mkubwa kuomba kura kwa wananchi wakati akiendelea na kampeni zake za kusaka kura katika Kata za Pemba na Kibati Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro.

Akizungumza na wananchi waliojitokeza kumsikiliza, Sara alisema wanawake wana maarifa makubwa ya kuhakikisha familia inapata chakula na ustawi, na akasisitiza kuwa endapo atachaguliwa kuwa Mbunge wa Mvomero, atayapeleka maarifa hayo bungeni kwa ajili ya kupigania maendeleo ya wananchi.

Sara mbali na kuomba kura kwaajili yake lakini alitumia majukwaa mbalimbali kila aliposimama kuomba kura aliomba kura kwaajili ya Mgombea wa Kiti cha Rais kupitia Chama chga Mapinduzi, Dkt. Samia Suluhu Hassan. 

Aidha akiwa Kata ya Mtibwa, Sara alimnadi Mgombea Urais wa CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan na kusema kuwa Rais Samia hawezi kufananishwa na marais wengine kutokana na namna alivyochukua madaraka baada ya kifo cha mtangulizi wake, Rais wa Awamu ya Tano Dkt. John Magufuli, na kuendelea kuiongoza nchi kwa hekima, busara na umakini.

Aidha, alibainisha kuwa Rais Samia ameonesha uthubutu mkubwa kwa kusimamia miradi mikubwa iliyoachwa na mtangulizi wake, huku akiibua na kusimamia miradi mipya inayolenga kuboresha huduma za kijamii na kukuza uchumi wa taifa.

Sara aliwaomba wananchi wa Mvomero na Watanzania kwa ujumla kuendelea kumuunga mkono Rais Samia ili kuhakikisha maendeleo hayo yanapata mwendelezo.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Mvomero, 
Teresphory Jacka akimnadi Mgombea Ubunge kupitia Chama hicho, Bi. Sara Msafiri katika moja ya mikutano yake ya kampeni. 


Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Mvomero, 
Teresphory Jacka akimnadi Mgombea Ubunge kupitia Chama hicho, Bi. Sara Msafiri katika moja ya mikutano yake ya kampeni. 





Posted by MROKI On Sunday, September 21, 2025 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo