Nafasi Ya Matangazo

January 29, 2026

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi akisalimiana na Meneja Ubunifu na Teknolojia kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dkt. Gerald Kafuku muda mfupi baada ya kumalizika kikao baina yao kilichofanyika katika Ofisi ndogo ya Ofisi ya Makamu wa Rais iliyopo Luthuli Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi akizungumza jambo wakati wa kikao baina yake na watendaji waandamizi wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) wakati wa kikao baina yao kilichofanyika katika Ofisi ndogo ya Ofisi ya Makamu wa Rais iliyopo Luthuli Jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi akimsikiliza Mratibu Utafiti Mwandamizi wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknoloja (COSTECH) Bw. Emmanuel Girimwa wakati wa kikao baina yao kilichofanyika katika Ofisi ndogo ya Ofisi ya Makamu wa Rais iliyopo Luthuli Jijini Dar es Salaam.
 Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi akiwa katika picha ya pamoja na Meneja Ubunifu na Teknolojia kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dkt. Gerald Kafuku muda mfupi baada ya kumalizika kikao baina yao kilichofanyika katika Ofisi ndogo ya OfisI ya Makamu wa Rais iliyopo Luthuli Jijini Dar es Salaam.   Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Dar teknohama, Bi. Patience Abraham.
*************
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi Watendaji Waandamizi wa COSTECH waliofika ofisini kwake kuwasilisha andiko la kitaalamu la mwongozo wa kisera kuhusu uendelezaji wa teknolojia ya matumizi ya magari  ya umeme.

Amesema matumizi ya teknolojia ya magari ya umeme imeshika kasi kwa sasa duniani na kuitaka COSTECH kuhakikisha inaandaa sera na miongozo mepesi kwa sekta binafsi ili iweze kushiriki kikamilifu katika mageuzi hayo.

“Ukienda katika mataifa mengi ya Bara la Ulaya kwa sasa, yanatumia sana teknolojia hii na sekta binafsi ndiyo kinara, wakati umefika sasa kwa Tanzania kuhakikisha sekta binafsi inapewa msukumo na fursa ya uwekezaji katika miundombinu hii” amesema Dkt. Muyungi.

Aidha amesema Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais itaendelea kuweka mazingira wezeshi na kuhimiza Wizara za kisekta na Taasisi zinazohusika katika uendelezaji wa teknolojia hiyo zinaimarisha ushirikiano wa karibu na COSTECH.

Ameongeza kuwa uwepo wa matumizi ya teknolojia ya magari hayo yatarahisisha juhudi za uhifadhi na utunzaji wa mazingira kwa kuwa tayari Serikali imefanikisha utekelezaji wa miradi mikubwa ya nishati ya umeme nchini.

Amesisitiza kuwa suala la matumizi ya teknolojia ya vifaa hivyo halina budi kwenda sambamba na kujenga uwezo kwa kuwapatia mafunzo wataalamu waliopo katika vyuo mbalimbali vya ufundi ikiwemo Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) , Chuo cha Taifa cha Usafirshaji (NIT) na Taasisi ya Teknlojia Dar es Salaam (DIT).

“Suala la Mafunzo na ujuzi ni muhimu, hivyo hatuna budi kuwawezesha na kupata maarifa ya kutosha yatakayosaidia katika usimamizi wa miundombinu ya teknolojia hizi” amesema   Dkt. Muyungi.

Amebainisha kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais kupitia Kituo cha Taifa cha Kuratibu Kaboni (NCMC) kitahakikisha kinashirikiana kwa karibu na COSTECH iili kuratibu vyema kuratibu matumizi ya teknolojia hizo ambayo ni kichocheo muhimu katika biashara ya kaboni. 

Kwa upande wake Meneja wa Ubunifu na Teknolojia- COSTECH, Dkt. Gerald Kafuku ameishukuru Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kuendelea kutoa ushauri na maelekezo ya kitaalamu yaliyowekeza uandaaji wa andiko la mradi huo.

Dkt. Kafuku amesema taarifa ya andiko hilo limekusudia kuandaa mitaala ya kozi fupi na za muda mrefu zitakazotolewa katika vyuo vya ufundi ikiwemo VETA, NIT), DIT na Chuo cha Ufundi Arusha- ATC.

Aidha amesema COSTECH pia imepanga kufanya mazungumzo na wadau mbalimbali wa kimataifa ikiwemo Serikali ya Norway hatua inayolenga kufanikisha upatikanaji wa mafunzo watakaosimamia miundombinu ya teknolojia hizo.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Watendaji Waandamizi wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknoloja wakiongozwa na Meneja Ubunifu na Teknoloja, Dkt.  Dkt. Gerald Kafuku (wa pili kushoto) muda mfupi baada ya kumalizika kikao baina yao kilichofanyika katika Ofisi ndogo ya Ofisi ya Makamu wa Rais iliyopo Luthuli Jijini Dar es Salaam.


Posted by MROKI On Thursday, January 29, 2026 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo