Meneja wa Ofisi ya Kanda ya Kati, Magdalena Mtenga (aliyesimama),
akiongea wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Usimamizi wa Maabara za Kemia kwa
Wakuu wa Shule za Sekondari wa Jiji la Dodoma (TAHOSSA) yaliyofanyika katika
Ukumbi wa Chuo cha Ualimu Bustani, Wilaya ya Kondoa, Mkoa wa Dodoma, Septemba
29, 2025.Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Sechelela Dodoma, ambaye ni Mwenyekiti wa Wakuu wa Shule za Sekondari (TAHOSSA), Grace Shilly, akimkaribisha Meneja wa Kanda ya Kati, Magdalena Mtenga (hayupo pichani) kwa ajili ya kufungua mafunzo ya Usimamizi wa Maabara za Kemia kwa Wakuu wa Shule za Sekondari kutoka Jiji la Dodoma (TAHOSSA) yaliyofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Ualimu Bustani Wilaya ya Kondoa,mkoani Dodoma, Septemba 29, 2025.
Mwakilishi wa Walimu Wakuu wa Kanda ya Kati (TAHOSSA), Peter Mlugu, akiishukuru Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa kutoa Mafunzo ya Usimamizi wa Maabara za Kemia kwa Wakuu wa Shule za Sekondari (TAHOSSA) wa Jiji la Dodoma yaliyofanyika katika Chuo cha Ualimu Bustani, Wilaya ya Kondoa, Septemba 29, 2025.
Mwakilishi wa Walimu Wakuu wa Kanda ya Kati (TAHOSSA), Peter Mlugu, akiishukuru Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa kutoa Mafunzo ya Usimamizi wa Maabara za Kemia kwa Wakuu wa Shule za Sekondari (TAHOSSA) wa Jiji la Dodoma yaliyofanyika katika Chuo cha Ualimu Bustani, Wilaya ya Kondoa, Septemba 29, 2025.
Mtumishi wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Kanda ya
Kati, Revocatus Mwamba, akiwasilisha mada juu ya Mfumo wa Ubora ndani ya
Maabara za Kemia, Usimamizi na uteketezaji wa Kemikali taka katika mafunzo ya Wakuu
wa Shule za Sekondari (TAHOSSA) wa Jiji la Dodoma yaliyofanyika katika Ukumbi
wa Chuo cha Ualimu Bustani, Wilaya ya Kondoa, Septemba 29, 2025.
Baadhi ya Walimu Wakuu
walioshiriki mafunzo wakiuliza maswali juu ya majukumu ya Mamlaka ya Maabara ya
Mkemia Mkuu wa Serikali katika mafunzo ya Usimamizi wa Maabara za Kemia kwa Wakuu wa Shule za
Sekondari (TAHOSSA) kutoka Jiji la Dodoma yaliyofanyika katika Chuo cha Ualimu
Bustani kilichopo Wilaya ya Kondoa, Mkoa wa Dodoma Septemba 29, 2025.
Wakuu wa Shule
wakijaza Dodoso la Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kuhusu taarifa
za Usimamizi wa Maabara za Kemia katika mafunzo kwa Wakuu wa Shule za Sekondari (TAHOSSA) wa Jiji la Dodoma yaliyofanyika
katika Ukumbi wa Chuo cha Ualimu Bustani, Wilaya ya Kondoa, Dodoma, Septemba
29, 2025.
Meneja wa Mamlaka ya
Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Kanda ya Kati, Magdalena Mtenga (watatu
kulia, Mstari wa Mbele), akiwa pamoja na viongozi wa Wakuu wa Shule za
Sekondari (TAHOSSA) kutoka wilaya za Dodoma, Chemba, Bahi, Chamwino, Kondoa DC,
Kondoa TC, Kongwa na Mpwapwa baada ya mafunzo ya Usimamizi wa Maabara
za Kemia katika Mkoa wa Dodoma
yaliyofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Ualimu Bustani Wilaya ya Kondoa, Mkoani
Dodoma, Septemba 29, 2025.



.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)



0 comments:
Post a Comment