Kiongozi wa Chama cha ACT
Wazalendo Doroth Semu amesema chama hicho kitashiriki kikamilifu katika
uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba mwaka huu licha ya baadhi ya vyama kutangaza
kutoshiriki uchaguzi huo.
Doroth ameyasema hayo leo
April 16 wakati alipokua akizungumza na waandishi wa habari mjini Unguja.
Amesema wameamua kushiriki
uchaguzi kuipa thamani kura za wananchi pamoja na kuwepo kwa changamoto nyingi
ambazo zimekua zikikandamiza ustawi wa demokrasia Nchini.
Amesema watatumia Uchaguzi
Mkuu 2025 kukabiliana na watawala vyovyote vile watakavokuja lakini hawatafanya
kabisa kosa la kususia.
"Tutaendelea kulinda
demokrasia na tupo tayari kupambana na yoyote yule," alisema.
Pamoja na hayo kiongozi huyo
wa Chama alisema wameamua kuja na maamuzi hayo baada ya kujifunza kwa kina
mataifa yanayosusia uchaguzi na madhara yake.
Aidha, amesema watautumia pia
uchaguzi huo kama jukwa la mapambano na kulinda demokrasia.
Katika hatua nyengine amesema
Chama cha Mapunduzi CCM wameshindwa kuwatoa watanzania walio wengi kwenye
dimbwi la umasikini ambao ndio kiu ya walio wengi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment