Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi Dk.Emmanuel Mkilia akizungumza na Jukwaa la Wahariri (TEF) ambapo amesema uwepo wa teknolojia umefanya taarifa kusambaa kwa kasi na haraka hivyo ni muhimu kuzingatia ulinzi wa taarifa binafsi.

TUME ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi(PDPC) iliyoanzishwa mwaka 2022 , imekutana na Jukwaa la Wahari Tanzania(TEF) kwa lengo la kukumbushana na kujengeana uelewa kuhusu umuhimu wa kuimarisha faragha za watu katika kuandika na kutoa habari zinazohusu taarifa za watu.
Akizungumza wakati wa semina hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi Dk.Emmanuel Mkilia amesema uwepo wa teknolojia umefanya taarifa kusambaa kwa kasi na haraka hivyo ni muhimu kuzingatia ulinzi wa taarifa binafsi.
“Zana ya ulinzi wa taarifa binafsi ni muhimu kwasababu inazungumzia udhibiti wa taarifa binafsi.Kuna kampuni kubwa zimepata hasara kwasababu ya kuvunja sheria ya taarifa binafsi, hivyo kutoeleweka kwa zana hii kunaweza kuleta madhara makubwa kwa mtu binafsi na hata kwa taarifa za nchi.
“Ulinzi wa taarifa binafsi ni muhimu ili kuzuia wizi wa taarifa binafsi.Ni vema tukaelewa zana nzima inayohusu usalama wa taarifa binafsi,”amesema na kuongeza anafahamu wahariri wanapotekeleza majukumu yao katika vyombo vya habari wanachakata taarifa kabla ya kwenda kwa umma, hivyo ni vema wakalinda taarifa binafsi.
“Ni wajibu wetu sote kuhakikisha tunazingatia ulinzi wa taarifa zetu ili kulinda faragha za watu.Hakuna anayependa faragha zake zitolewe hadharani na maisha ni drama maana kuna nyuma ya pazia na katika stage.
“Hakuna anayependa ujue anayofanya nyuma ya pazia ,hivyo unaweza kuona umuhimu wa jambo hili tunalozungumzia.Tuhakikishe jamii inaelewa umuhimu wa kulinda faragha za watu kwani tuko katika dunia ya kidigitali.Mnaona siku hizi kituko chochote kikitokea kinasambaa kwa kasi sana, kwa hiyo ,mnaweza kuona msingi wa ulinzi wa taarifa binafsi.
“Niseme machache katika jambo hili, tume hii imesimama katikati ya teknolojia na maisha ya watu, tumejaribu kuangalia maisha ya watu wanavyoishi, lakini teknolojia haina siri, haina hisia lakini mwisho wa siku tunamuangalia huyu mtu ambaye anatumia teknolojia, kwa hiyo tunalojukumu la kulinda hisia.
“Warsha hii inatoa fursa kujifunza na kujengeana ulewa wa kina jinsi ya kulinda faragha za watu katika kazi zenu za habari. Warsha hii ni mwanzo maana jukumu letu kubwa ni taarifa kwa umma.Tutaendelea kutumia jukwaa hili ili kuhakikisha watu ambao tumepanga kuwafikia wajue mambo ya msingi kuhusu taarifa binafsi.
“Na sisi tume sehemu kubwa ya kazi yetu ni elimu kwa umma, hivyo kwa kupitia jukwaa hili la wahariri ndio silaya yetu muhimu ya kuitumia kuifikia jamii inaelewa umuhimu wa kulinda faragha za watu.”
.jpeg)
.jpeg)




.jpeg)
.jpeg)
Source: Michuzi Blog
0 comments:
Post a Comment