Nafasi Ya Matangazo

February 22, 2025












Maneno hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi ,Ofisi ya Waziri Mkuu anayesimamia Kazi, Vijana , Ajira na Wenye Ulemavu Ndg. Ridhiwani Kikwete wakati akimkaribisha Dr. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania azungumze na waliojitokeza katika sherehe za maadhimisho ya miaka 10 ya Mafunzo ya Wanawake Viongozi na kutoa vyeti kwa wahitimu wa kozi hiyo kwa mwaka 2024/25.

Katika Risala yake, Mh. Rais Samia pamoja kuwapongeza wahitimu na alitumia kuwanasaa wahitimu kutambua nafasi zao katika jamii wanayoishi pasi kusahau kuwa kama wanawake ndiyo walezi wa Jamii na hivyo wasije geuka kuwa wavurugaji wa jamii kwa sababu ya ukubwa wa elimu yao na madaraka waliyonayo.

Katika sherehe hizo wahitimu zaidi ya 110 walitunukiwa vyeti. Kiongozi wa Wahitimu hao Bi. Adeline Mushi alimshukuru Mh. Rais kwa kushiriki nao na kuwa jicho ya  programu hiyo toka ilivyoanza. Na wahitimu kwa upande mwengine walitoa zawadi kwa mkoa wa Dar Es Salaam kwa kuchangia vifaa vya kusaidia watoto wadogo wanaozaliwa.

Programu hii inayoendeshwa kwa ushirikiano baina ya Taasisi ya Waajiri Tanzania (ATE) na shirikisho la Waajiri Norway (NHO) linalenga kuwawezesha wanawake waliokwenye Uajiri kuongeza ujuzi wa Utawala na Usimamizi -Uongozi ili kuweza kushiriki katika Uongozi na ngazi za Juu za Usimamizi wa Bodi/ Taasisi na Mashirika mbalimbali. Washiriki wa kozi hiyo wamekuwa wakiongezeka toka kozi ilipoanzishwa miaka 10 na mafanikio yake ni makubwa sana.
Posted by MROKI On Saturday, February 22, 2025 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo