Nafasi Ya Matangazo

February 20, 2025




Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mlezi wa CCM kwa Mikoa ya Kusini na Kaskazini Unguja, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amesema kuwa CCM imejipanga kikamilifu kuhakikisha inaendelea kushika dola katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, kwa kuwa kazi iliyofanywa na Serikali inatosha kutangaza sera za ushindi.

Dkt. Tulia ametoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na Wanachama wa CCM katika Ukumbi wa CCM Hanyegwamchana, mara baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi katika Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar, leo tarehe 20 Februari 2025. Ziara hiyo ililenga kukagua miradi mbalimbali ya CCM pamoja na kuwaeleza wananchi kuhusu malengo ya CCM katika mkoa huo.

Aidha, Dkt. Tulia amewahimiza vijana wa CCM wenye sifa za kugombea nafasi mbalimbali za Uongozi kujitokeza kwa wingi, ili waweze kuonesha uwezo wao na kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa taifa. Amesisitiza kuwa CCM ina sera shirikishi zinazotoa fursa kwa kila mtu wakiwemo vijana, kushiriki katika Uongozi na maendeleo ya nchi.

“Ndani ya Chama hiki tunaunganishwa na imani yetu. Kipindi cha Uchaguzi si muda wa kunyoosheana vidole au kuoneshana ubaya, bali ni wakati muhimu wa kushikamana ili kupata ushindi wa kishindo. Hiyo ndiyo sera yetu kuu,” amesema Dkt. Tulia.
Posted by MROKI On Thursday, February 20, 2025 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo