
Mhe. Simbachawene
amesema hayo leo jijini Dodoma wakati akizindua Bodi ya Kima cha Chini cha
Mshahara katika Utumishi wa Umma.
Mhe.
Simbachawene amesema Kima cha Chini cha Mshahara ni suala muhimu sana na
lisiposhughulikiwa vizuri linaweza kusababisha migogoro isiyo ya lazima na
hivyo kuzorotesha uchumi na maendeleo ya nchi kwa ujumla.
Ameongeza
kuwa, Kima cha chini cha mshahara kisichozingatia hali halisi ya uchumi ni
hatari katika maendeleo ya nchi hasa kutokana na ukweli kwamba kunaweza
kusababisha kutokea kwa mfumuko wa bei, na kuongeza gharama za uendeshaji.
Waziri
Simbachawene amesema Bodi ya Mshahara katika Sekta ya Umma ina jukumu la
kufanya uchunguzi na kupendekeza kwa Waziri mwenye dhamana na masuala ya
Utumishi wa Umma kuhusu Kima cha Chini cha Mshahara katika Sekta ya Umma, hivyo
katika kutekeleza majukumu haya, Bodi ina wajibu wa kuzingatia maslahi ya nchi
na mustakabali wa uchumi wa nchi wakati wa kutoa mapendekezo stahiki.
Kwa Upande
wake, Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI ambaye ni Mkurugenzi wa
Idara ya Uendelezaji wa Taasisi, Bw. Nolasco Kipanda amesema pamoja na uzinduzi
wa bodi hiyo, Wajumbe watapatiwa mafunzo kwa ajili ya kujengewa uwezo zaidi na
kupata uelewa kuhusu majukumu ya upangaji wa kima cha chini cha mshahara katika
Utumishi wa Umma.
Naye Mwenyekiti
wa Bodi ya Kima cha Chini cha Mshahara katika Utumishi wa Umma, Bw. Mathias
Kabunduguru amemuahidi Waziri Simbachawene kuwa watatekeleza majukumu yao kwa
ufanisi na malengo yaliyokusudiwa katika kupendekeza na kutoa ushauri kwa
ustawi wa nchi.
Uteuzi wa
Bodi ya Kima cha Chini cha Mshahara umefanywa kwa mujibu wa Kifungu cha 35(1)
cha Sheria ya Taasisi za Kazi Na. 7 ya mwaka 2004 na kufanyiwa marekebisho
kupitia kifungu cha 14(b) cha Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Ajira na Kazi
(The Employment and Labor Laws (Miscellaneous Amendment Act) Na. 24 ya mwaka
2015.
Kupitia Marekebisho hayo yaliyopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 08/07/2015, Serikali ilianzisha Bodi mbili, moja kwa ajili ya Sekta binafsi na nyingine kwa ajili ya Sekta ya Umma. Marekebisho hayo yalilenga kuboresha ufanisi na kupunguza gharama za uendeshaji.
0 comments:
Post a Comment