Mkurugenzi Msaidizi Sehenu ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu Wizara ya Nishati, Bi. Bahati Mtono amesems Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imeondoa changamoto waizokutana nazo wanawake katika umiliki wa ardhi na masuala ya uongozi.
Bahati ameyasema hayo alipokuwa akielezea historia ya mwanamke katika kutetea haki zake katika kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.
"Historia inaonesha miaka ya 1910 kulikuwa na harakati mbalimbali ambapo wanawake walijipanga kupigania haki zao na mwaka 1975 Umoja wa Mataifa ulianzisha siku ya Wanawake Duniani." Amesema Bi. Mtono
Ameeleza kuwa, lengo hasa la kuanzisha siku hiyo ni kupambania haki za mwanamke na kuikumbusha Dunia kuhakikisha inazingatia wanawake katika upatikanaji wa haki za msingi lakini pia masuala ya usawa wa kijinsia kati ya wanawake kuhakikisha wote wanapata haki zao za msingi.
Amesema Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati zinajitahidi kusaidia wanawake akitolea mfano Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kupitia mradi wa TAZA ambapo kama sekta inajitahidi kuongeza wanawake wahandisi.
Kwa upande wa kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia ameipongeza Serikali kwa kuweka nguvu katika programu ambayo Wizara ya Nishati inaipa kipaumbele ili kuwezesha asilimia 80.ya Watanzania kutumia nishati safi ya kupikia ifikapo 2034.
Amesisitiza kuwa kupitia programu ya nishati safi ya kupikia mwanamke anakwenda kukombolewa kiuchumi kwa kuokoa muda wa kutafuta nishati na hivyo kushiriki katika masuala mbalimbali ya kijamii .
0 comments:
Post a Comment