Nafasi Ya Matangazo

February 22, 2025

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Cypriana Luhemeja akiifariji familia ya aliyeshiriki tukio la kuchanganya udongo wa iliyokuwa Tanganyika na Zanzibar Marehemu Bi. Sifael Mushi. Marehemu Bi. Sifael Mushi ambaye amefariki dunia Februari 20, 2025.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Cypriana Luhemeja akiifariji familia ya aliyeshiriki tukio la kuchanganya udongo wa iliyokuwa Tanganyika na Zanzibar Marehemu Bi. Sifael Mushi. Marehemu Bi. Sifael Mushi ambaye amefariki dunia Februari 20, 2025.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Cypriana Luhemeja akisaini kitabu cha maombolezo alipowasili eneo la Makongo Jijini Dar es Salaam leo Februari 22, 2025 kwa ajili ya kutoa pole na kuifariji familia ya aliyeshiriki tukio la kuchanganya udongo wa iliyokuwa Tanganyika na Zanzibar Marehemu Bi. Sifael Mushi ambaye amefariki dunia Februari 20, 2025.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Cypriana Luhemeja (katikati) akiwa katika katika picha ya pamoja na familia ya Marehemu Sifael Mushi aliyeshiriki tukio la kuchanganya udongo wa iliyokuwa Tanganyika na Zanzibar, nyumbani Makongo Juu Jijini Dar es Salaam leo Februari 22, 2025.

Sehemu ya waombolezaji nyumbani Makongo Juu Jijini Dar es Salaam kufuatia kifo cha aliyeshiriki tukio la kuchanganya udongo wa iliyokuwa Tanganyika na Zanzibar Marehemu Bi. Sifael Mushi ambaye amefariki dunia Februari 20, 2025.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Cypriana Luhemeja (katikati) akiwa katika akiwa na Naibu Karibu Mkuu (Muungano) Bw. Abdallah Hassan Mitawi (wa pili kulia), Mkurugenzi wa Muungano Dkt. Juma Mohamed Salum na ndugu wa Marehemu Sifael Mushi aliyeshiriki tukio la kuchanganya udongo wa iliyokuwa Tanganyika na Zanzibar, wakati wa ibada ya fupi nyumbani Makongo Juu Jijini Dar es Salaam leo Februari 22, 2025.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Cypriana Luhemeja ametoa wito kwa Watanzania kuendelea kudumisha na kutunza historia ya Muungano kwa vizazi vya sasa na vijavyo ili kuwaenzi waasisi wake.

Ametoa wito huo wakati akizungumza na waombolezaji eneo la Makongo Juu Jijini Dar es Salaam leo Februari 22, 2025 Jijini Dar es Salaam, alipofika kutoa pole na kuifariji familia ya aliyeshiriki tukio la kuchanganya udongo wa iliyokuwa Tanganyika na Zanzibar Marehemu Bi. Sifael Mushi ambaye amefariki dunia Februari 20, 2025.

Akitoa salamu za Serikali, Mhandisi Luhemeja amesema Marehemu Sifael alikuwa ni mtu muhimu katika historia ya Muungano wakati wa tukio la kuchanganya udongo lililkofanyika Aprili 26, 1965 ikiwa ni mwaka mmoja baada ya kuasisiwa kwa Muungano Aprili 26, 1964.

Akiifariji familia ya marehemu amesema pamoja na majonzi ya kumpoteza mpendwa wao, ina bahati ya kupata mtu aliyeshuhudia Muungano ambao umedumu hadi leo.

“Niwaombe tuudumishe Muungano kwani wengi wetu tumezaliwa baada ya Muungano hivyo ni vyema tukaendelea kuitunza historia yake namna alivyoshiriki katika tukio lile la kuchanganya udongo, ni nadra sana kumuona Mtanzania mmoja ana picha ya Rais wa Awamu ya Sita, wa Awamu ya Tano, Awamu ya Nne na Awamu ya Kwanza si jambo rahisi, lakini kwa Marehemu Sifael tunalishuhudia,” amesema.

Marehemu Sifael ambaye alikuwa miongoni mwa vijana wa Kitanzania walishiriki katika tukio la kuchanganga udongo wa Tanganyika na Zanzibar, alifariki dunia katika Hospitali ya Mzena Jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.

Wengine walioshiriki katika tukio hilo na wametangulia mbele ya haki ni Marehemu Hassanieli Mrema aliyefariki Mei 04, 2024, Marehemu Khadija Abbas Rashid alifariki Agosti 22, 2023 na Marehemu Omar Hassan Mkele alifariki Agosti 28, 2024.

 

 

 

 

 

Posted by MROKI On Saturday, February 22, 2025 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo