Nafasi Ya Matangazo

October 12, 2024

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo ameshiriki zoezi la Uandikishaji kwenye Daftari la Wapiga kura kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Kitongoji cha Kimani wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani leo Oktoba 12,2024.
***********
Na.Alex Sonna-KISARAWE
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo ameshiriki zoezi la Uandikishaji kwenye Daftari la Wapiga kura kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Kitongoji cha Kimani wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani.

Akizungumza leo Oktoba 12,2024 mara baada ya kujiandikisha Mhe.Dk.Jafo amewahimiza wananchi wa Kisarawe kujitokeza kwa wingi na kujiandikisha katika vituo vya kujiandikisha wapiga kura ili waweze kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024.

Dk.Jafo amesema zoezi la kujiandikisha katika daftari la kupiga kura ni muhimu kwa kuwa ni wajibu kushiriki katika kuchagua viongozi watakaoweza kuwasaidia wananchi.

"Viongozi wa serikali za mitaa ndiyo wanaoishi jirani zaidi na wananchi hivyo ni muhimu kushiriki katika kuwachagua wale watakaolinda maslahi ya jamii husika."amesema Dk.Jafo

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo ameshiriki zoezi la Uandikishaji kwenye Daftari la Wapiga kura kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Kitongoji cha Kimani wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani leo Oktoba 12,2024.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo, akijiandikisha kwenye Daftari la Wapiga kura kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Kitongoji cha Kimani wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani leo Oktoba 12,2024.
Posted by MROKI On Saturday, October 12, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo