Nafasi Ya Matangazo

October 12, 2024




🔴Rais Samia Suluhu Hassan kufunga maonesho
Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde amepongeza maonesho ya 7 ya Teknolojia ya Madini mkoani Geita kwa kuendelea kukua na kuongeza idadi kubwa zaidi ya washiriki wa ndani na nje ya nchi na hivyo kufikisha idadi ya zaidi ya washiriki 800 kwa mwaka huu 2024 na hivyo kuutaka mkoa wa Geita kuimarisha miundombinu ya eneo la
Maonesho ili kuyafanya ya Kimataifa.

Waziri Mavunde ameyasema hayo leo Geita,wakati akikagua maonesho na kutoa hati za pongezi,ushiriki na ushindi kwa waoneshaji wa bidhaa na huduma.

“Ni dhamira ya Serikali kuona maonesho haya yanakuwa na kufikia hadhi ya kimataifa,hivyo Wizara ya Madini na Mkoa wa Geita tutashikiriana kwa ukaribu ili azma na ndoto hii kutimia.

Maonesho ya mwaka huu yamevutia udhamini mkubwa na ushiriki wa wadau wengi sana wa nje na ndani ya nchi,na hii ni dalili njema ya ukuaji wa maonesho haya mwaka hadi mwaka”Alisema Mavunde

Akitoa salamu zake,Mkuu wa Mkoa wa Geita amewapongeza washiriki wote wa mwaka huu kwa kuwa mahiri na wabunifu na hivyo kuyafanya maonesho haya kuvutia watu wengi wakiwemo wageni kutoka nchi mbalimbali.

Mh Shigela pia ameeleza mkakati wa mkoa ni kujenga miundombinu ya kudumu na kuboresha eneo la maonesho ili kukidhi mahitaji ya kimataifa.

Maonesho haya ya 7 ya Teknolojia ya Madini mkoani Geita yanafikia tamati tarehe 13.10.2024 kwa kuhitimishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia S. Hassan ambaye anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi.
Posted by MROKI On Saturday, October 12, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo