Nafasi Ya Matangazo

October 08, 2024

Lucy Mbogoro, Meneja wa Uhusiano wa Umma na Masoko wa TANTRADE akizungumza katika banda hilo. 
***********
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) imeungana na Halmashauri ya Wilaya ya Geita kuratibu Maonyesho ya Teknolojia ya Madini kwa mwaka 2024, ambayo yameendelea, Oktoba 7, 2024, katila viwanja vya EPZ Bombambili mjini Geita.

Maonyesho haya, yanayofanyika kwa mara ya saba, yanawalenga wafanyabiashara wa madini, Wachimbaji na wadau wengine muhimu katika sekta ya madini.

Akizungumza na waandishi wa habari, Lucy Mbogoro, Meneja wa Uhusiano wa Umma na Masoko wa TANTRADE, ameeleza kuwa TANTRADE imeanzisha "Kliniki ya Biashara" kwa kushirikiana na taasisi za umma kama SIDO, BRELA, TRA, TMDA, Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali na wadau wengine. 

Lengo la kliniki hii ni kuwawezesha wafanyabiashara wa madini wa Geita na wengine kutoka maeneo mbalimbali nchini kupata elimu na ushauri unaohusu biashara zao, hususan namna ya kupanua masoko yao hadi kimataifa na kushirikiana na wafanyabiashara wakubwa.

Mbogolo amesisitiza kuwa kliniki hiyo inalenga pia kutoa majibu kwa maswali na changamoto mbalimbali zinazowakabili wafanyabiashara wa madini.

Kupitia banda la TANTRADE, wafanyabiashara wataweza kujifunza na kupata ushauri wa moja kwa moja kutoka kwa wataalam na wadau mbalimbali waliopo kwenye maonyesho hayo.

Aidha, TANTRADE imeanzisha eneo maalum kwenye maonyesho hayo linaloitwa "Made in Tanzania", ambalo linatenga nafasi kwa wafanyabiashara wanaotengeneza bidhaa za ndani ya nchi.

Eneo hili lina lengo la kuwasaidia wafanyabiashara hao kuonyesha bidhaa zao na kupata fursa za kibiashara ndani na nje ya nchi.
Marcelina Anthony Afisa Biashara Mwandamizi TANTRADE akimsikiliza mmoja wa wananchi waliotembelea katika kliniki ya Biashara katika maonesho ya Tenknolojia ya madini mjini Geita. 
Lucy Mbogoro, Meneja wa Uhusiano wa Umma na Masoko wa TANTRADE akionesha baadhi ya bidhaa zilizotengenezwa Tanzania katika banda hilo. 
Nsajigwa Wilfred Afisa Uhusiano wa I'mma Mkuu FCC akitoa maelezo kwa mmoja wa wananchi waliotembelea katika banda hilo. 
 Nsajigwa Wilfred Afisa Uhusiano wa I'mma Mkuu FCC akitoa maelezo kwa Unice Matanyanga Afisa Biashara wilaya ya Nyag,'wale aliotembelea katika banda hilo. 
Posted by MROKI On Tuesday, October 08, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo