Nafasi Ya Matangazo

October 28, 2024

Mkutano wa Kumi na Saba wa Bunge utaanza kesho Jumanne tarehe 29 Oktoba 2024 na kumalizika tarehe 8 Novemba 2024 Jijini Dodoma.
 Shughuli ambazo zinatarajiwa kufanyika wakati wa Mkutano huu ni pamoja na;

1.0 Kupokea na kujadili taarifa za Kamati za PAC, LAAC NA PIC
Katika Mkutano huu, Bunge litapokea uchambuzi wa Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) uliofanywa na Kamati ya Kudumu ya Bunge za Hesabu za Serikali (PAC) na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) kuhusu Hesabu zilizokaguliwa kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023. Aidha Bunge pia litapokea na kujadili Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) kuhusu Uwekezaji wa Mitaji ya Umma kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023.
 
2.0 Bunge kukaa kama Kamati ya Mipango
Mkutano huu ni mahsusi kwa ajili ya kupokea, kujadili na kushauri kuhusu Mapendekezo ya Mpango wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali katika Mwaka wa Fedha 2025/2026. Aidha, Bunge litashauri kuhusu mwongozo wa uandaaji bajeti, vyanzo vya mapato, utekelezaji na vipaumbele vya mpango huo.
 
3.0 Maswali
Katika Mkutano huu wa Kumi na Saba, wastani wa maswali 160 ya Kawaida yanatarajiwa kuulizwa na kujibiwa na Serikali Bungeni. Aidha, wastani wa Maswali 16 ya papo kwa papo kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu yanatarajiwa kuulizwa kwa siku za Alhamisi.
 
Ratiba ya Shughuli za Mkutano wa Kumi na Saba inapatikana katika tovuti ya Bunge www.bunge.go.tz
Posted by MROKI On Monday, October 28, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo