Nafasi Ya Matangazo

September 06, 2024





Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imehitimisha mafunzo ya siku tatu kwa watumishi wa wizara hiyo kuhusiana na viashiria hatarishi.

Mafunzo hayo yamefanyika jijini Dodoma yakihusisha Wakuu wa Idara na Vitengo pamoja na Waratibu wanaosimamia masuala ya viashiria hatarishi kwenye wizara.

Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Seushi Mburi amesema mafunzo hayo yanatokana na maelekezo ya Serikali kwa wizara na taasisi zote za serikali kuandaa daftari la viashiria hatarishi vitakavyosaidia katika utekelezaji wa majukumu sambamba na kuwa muongozo kwa wizara katika kutekeleza majukumu yake.

Kwa upande wake Mkaguzi Mkuu wa Ndani Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mwezeshaji wa Mafunzo hayo Bw. Alphonce Muro amesema, lengo la mafunzo hayo ni kutekeleza  azma ya serikali ya kuhakikisha kila taasisi inakuwa na mfumo madhubuti wa kusimamia viashiria hatarishi vinavyoweza kuzuia wizara isifikie malengo yake.

Naye mshiriki wa mafunzo ambaye pia ni Msajili wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya Bi. Stellah Tulo amesema, mafunzo yamewasidia kujifunza namna ya kutambua viashria hatarishi vinavyoweza kujitokeza pale wanapokuwa katika utekelezaji wa majukumu yao. 
Posted by MROKI On Friday, September 06, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo